Ubabe wa watawala wajinga

NANCA

Member
Joined
Jun 23, 2023
Posts
92
Reaction score
100
Kuna watu tena unakuta ni viongozi tena labda ni wa CCM tena unakuta labda ni mbunge, unakuta anatumia mamlaka yake kupokonya na kudhrumu viwanja vya wanyonge kwa kisingizio cha miradi. Unakuta anakshurutisha Mkurugenzi kuwaambia muyaache maeneo sababu kuna mradi kumbe ni mbunge amelipenda eneo. Unakuta anatumia vitisho hata kukutumia majambazi au kukuharibia kazi kisa tu amelitaka eneo lako na ww umegoma, analazimisha umuuzie tena kwa bei ya kutupa, unakataa anaanza kukuwinda.

- Sasa ndugu mweshimiwa rais wa Jamhuri ya muungano, Samia Suluhu Hassan embu tuambie Kama ardhi yote nchi hii ni mali ya wana CCM na wabunge wako, utuambie kua sisi maskini hatuna haki ya kumiliki maeneo ya kuvutia ila ni nyie wana CCM na wabunge wako, Rais utuambie kua sisi hatuna haki ya kuandaa maisha ya watoto wetu na hatma zao ila hao nyie wana CCM na wabunge wako, utuambie kua sisi watoto wetu ni nguruwe ila nyie wenu ndo binadamu.

Maana Kuna Mbunge yeye haridhiki karibu kila mahala ktk halmashauri hii anapataka yy hata kusingizia vimiradi visivyo na kichwa, anatisha watu na kuyanunua maeneo yao kwa lazima eti ukiuliza anasema yy ameipigania halmashauri kupata maendeleo. Basi mseme ili wengine tuhame tuwaachie nyie wana CCM.

- Sasa mimi binafsi Kuna mbunge anajipendekeza kibabe kulitaka eneo langu na uvumi umeanza, ana maeneo lundo lkn haridhiki. Sasa mimi aneo langu halipati, kwanza kama anatisha watu kwa mtutu basi mimi sifi na eneo halipati. Mungu yupo mrangoni kwangu sasa muendelee na dharuma zenu na dhuruma zake, Yani tuwachague wenyewe afu na ubabe mtuletee. Siku mimi nkifa kwa sbbu ya eneo lile basi watakao kua wameniua malipo watayapa.

- Sasa rais Samia Suluhu Hassan waambie wabunge wako kua ata sisi tumawatoto tunaowapigania hatma zao ili kesho yao kua nzuri, nchi haiwezi kuendelea Kama watu wachache wakiweko wabunge wako watataka kila kitu wamiliki wao. Wao wapambane na vitu vikubwavikubwa na wakubwa wenzao. Hakauna ataepata kipande cha ardhi yangu, na yeyeote ataetaka kunisogelea kwa ubabe Mungu amchukue hata kabla hajatoa mguu wake kunifikia, amlaani yy na kizazi chake cha kibabe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…