DOKEZO GE2025 Rushwa na ubabe watawala uchujaji wa wagombea CCM Moshi Vijijini

DOKEZO GE2025 Rushwa na ubabe watawala uchujaji wa wagombea CCM Moshi Vijijini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

MALLE JR

Member
Joined
May 7, 2025
Posts
9
Reaction score
4
Mchakato wa uchujaji wa wagombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini umetawaliwa na tuhuma nzito za rushwa, upendeleo na ubabe wa viongozi, hali iliyopelekea sintofahamu kubwa na kuibua mjadala mkali miongoni mwa wanachama wa chama hicho.

Kwa mujibu wa duru kutoka ndani ya mchakato huo, wajumbe 16 wa vikao vya kamati ya siasa na maalum vya maadili waliitwa kwa faragha kwenye moja ya hoteli ya kifahari usiku wa manane ambapo kila mmoja alidaiwa kupokea kiasi cha shilingi milioni moja kutoka kwa mgombea mmoja mwenye nguvu ya kifedha. Taarifa hizi zimevuja na kusambaa kwa kasi, zikizua maswali mengi kuhusu uhalali wa mchakato huo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Mzee Siril Mushi, ndiye anatajwa kuongoza vikao hivyo vya maadili. Chanzo kutoka ndani ya kikao hicho kinaeleza kuwa mwenyekiti huyo alionekana akiwa na chuki binafsi dhidi ya baadhi ya wabunge, huku akitumia lugha ya ubabe na vitisho kwa baadhi ya wajumbe, hali iliyodhoofisha uhuru wa kutoa maoni na kupendekeza wagombea kwa haki.

Katika mazingira hayo tata, taarifa zinaeleza kuwa Mbunge wa sasa wa Moshi Vijijini, Prof. Patrick Aloyce Ndakidemi, hakupendekezwa tena licha ya kuwa na rekodi ya utumishi. Vuta nikuvute kubwa pia inaripotiwa kuhusu jina la Mbunge wa Vunjo, Mhe. Dkt Charles Stephen Kimei, ambalo linadaiwa kuzua mgawanyiko mkali miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.

WITO WA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Wanachama wa CCM pamoja na wapenda demokrasia nchini wameanza kuhoji hatma ya mchakato huu na nafasi ya chama hicho katika kulinda maadili yake. Wito umetolewa kwa viongozi wa juu wa CCM kuchukua hatua za haraka kuchunguza tuhuma hizi nzito, kurejesha imani ya wanachama, na kuhakikisha haki inatendeka bila upendeleo wala vitisho.

Mchakato wa ndani ya chama ni msingi wa siasa safi – tukikubali kuubomoa kwa hongo na chuki binafsi, basi tunabomoa msingi wa utawala bora.
 
Mkiambiwa
NO REFORMS NO ELECTION
Mnasema watu wakatwe vichwa haya sasa unaona. kisu kimegusa mfupa
Huko KIBAMBA BI ANGELA KAIRUKI anagawa 70000 kwa kila mjumbe ili achaguliwe kuwa mbunge
Yaani unatoa pesa ili uchaguliwe kuwaletea watu maendeleo?
Hiyo ndiyo CCM
 
Uongozi wa juu ulijichagua wenyewe kupata nafasi za kugombea uongozi wake nchi na si kwa ridhaa ya wajumbe. Hakuna hatua yeyote itakayochukuliwa hapo.

karibu tutaongea lugha moja “No Reforms No Election”.
 
CCM inanuka Rushwa, Samia Mtoa na mpokea Rushwa. Majimbo yote hakuna Jimbo Wana CCM hawatoi Rushwa. Dawa ni kuwa na Uchaguzi huru na WA haki kupitia reforms
 
Huyu NDAKIDEMI amewahi kufanya nn tangu achaguliwe? Hata bungeni kulisemea jimbo hamna.
 
Back
Top Bottom