Twendeni tukawinde

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,938
Reaction score
61,728
Wikiend hii sitaki kutembelea maeneo ya starehe kabisa, bali nataka niitumie vizuri kwa kuwinda vindege mbalimbali; kama nitapata kanga, njiwa, kwelea kwelea, kware n.k sawa tu, na kama nitabahatisha wanyama wadogowadogo itakuwa vizuri pia.

Hapa nimeandaa manati, ndala za matairi (katambuga), kaptula ngumu ya jinsi na shati gumu la kadeti, kibuyu cha maji, na mahindi ya kukaanga.

Nimepanga katika uwindaji huu, niende na mdada mmoja machachari wa jf angalau na yeye akajifunze namna ya kutumia manati.

Kama kuna wazoefu wa kuwinda humu, tukutane mbugani na manati zenu.


 
Kuna siku nilichukua vijana wangu tukaenda kulowa mudfish mtoni tukashka had kobe wa maji yaan watoto walifurahi had sasa ukiwapa option ya kwenda kulowa sama au kuwinda ndege na kwenda kuogelea wanachagua uwindaji. Nakumbuka hiyo cku napita kamsitu flani kadogo kanga huyu hapa amelalia mayai nikamtega bila wao kujua mda kidogo narud nakuta kanasa vijana wakafurahi hadi wakasahau samaki wao. Mayai nilibeba yote nkamuekea kuku nikapata vifaranga 5 hadi leo kanga home hawakosi.
Nenda ndugu ukawinde japo utaambiwa ni uwindaji haram
 
kanga huwa wanatagia juu ya mti au chini?
 
Hii mipango yako imenichekesha sana 😂😂. Umeandaa vifaa mpaka mtu anaweza kudhani unaenda expedition ya National Geographic, kumbe ni manati na mahindi ya kukaanga. 😂

Ila hiyo ya kumpeleka mdada wa JF akajifunze kutumia manati ndiyo imenifanya nicheke zaidi. Muhimu tu msije mkawa wawindaji wa ndege mkawa wawindwaji na mwenye mbuga. 😂

Na usisahau, kanga, njiwa na kwelea ni viumbe hai pia—uwindaji uwe wa kisheria na kwa usalama, sio kugeuza weekend kuwa kesi ya polisi. 😅

Weekend njema, Equation X. Ukirudi na hadithi ya jinsi ulivyowinda mahindi badala ya kwelea, tutakusikiliza. 😂🔥
 
Kwa mfano, kwelea kwelea akipita kwenye paa la jengo langu, siruhusiwi kumuwinda?
 
Nimepata vijana wakutembeza kahawa, kuchomwa mahindi na kutembeza barafu mkuu, niku konekt kaka🤣🤣
Utakuwa umefanya vizuri sana
  • Vijana 100 wa kuuza kahawa- kwa siku kila mmoja aniletee 5,000
  • Vijana 500 wa kuuza barafu-kwa siku kila mmoja alete mauzo 50,000
  • Vijana 50 wa kuchoma mahindi- kwa siku kila kijana aniletee 5,000

Kwa siku nitakuwa naingiza shilingi= (100x 5,000) + (50,000 x 500) + (50 x 5000)
=500,000+ 25,000,000 + 250,000
= 25,750,000/= kwa siku

Umeona mapato kwa siku yatakavyokuwa?
 
Kaka unajua we ni akili kubwa na Huwa nakufatilia sana lengo langu nikuhakikisha naingiza laki tano Kwa siku kama faida ili nianze kisafiri, inshaallah unajua nataka nisafiri sana pande zote za dunia kaka
 
Kaka unajua we ni akili kubwa na Huwa nakufatilia sana lengo langu nikuhakikisha naingiza laki tano Kwa siku kama faida ili nianze kisafiri, inshaallah unajua nataka nisafiri sana pande zote za dunia kaka
Inawezekana kabisa, mfano mtu yuko Arusha/Moshi, kuna haja gani ya kwenda Dar na kutumia zaidi ya masaa 10 barabarani, wakati hapo Nairobi unaweza kutumia masaa 5 tu.
Muhimu ni kujitambua katika hii dunia unataka nini.
Pia katika kufanya biashara, si lazima kufanya kama wengine wanavyofanya ata kama biashara zinafanana. 'Do it in an uncommon way'​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…