Kwa wapenzi wa TV Series, hususani ambazo ni Political Thriller bila shaka wanaifahamu vizuri 24 Season 8. Kwa kifupi, 24 Season 8 inamzungumzia Rais Omari Hassan kutoka fictitious country; Kamistan. Ukiiangalia kwa haraka haraka, unaweza kuhadaika kwamba wanaizungumzia nchi somewhere karibu na Russia with those "…stan" stuff like Afghanistan, Pakistan, Turkmenistan, Kazakhstan, n.k. Hata hivyo, haiwezi kukuchukua muda kugundua kwamba wanaizungumzia Iran!
Kilichonivuta kuandika haya ni mfanano uliopo kati ya Series 24 Season 8 na yanayotokea sasa katika US-Iran Relationship hususani linapokuja suala la nuclear. Ikumbukwe kwamba, filming ya 24 Season 8 ilikuwa May 27, 2009; miaka mine kabla ya kuchaguliwa kwa Rais wa sasa wa Iran. Pamoja na tofauti hiyo kubwa ya muda; bado kuna ufananaji mkubwa katika Series hii na yale yanayoendelea.
- Wakati filming ya 24 Season 8 ilianza May 27, Rais wa sasa wa Iran alijiandikisha as Presidential Candidate on May 07.
- Kama nilivyosema hapo awali, 24 Season 8 inazugumzia fictitious country inayoitwa Kamistan ambayo Rais wake ni Omari Hassan, commonly referred as President Hassan; miaka minne baadae akaja Rais mpya wa Iran anayeitwa Hassan Rouhan!
- Hata hivyo, hoja ya msingi ni uamuzi wa Rais wa fictitious country, President Omar Hassan. Baada ya USA na Kamistan kuwa maadui kwa miongo kadhaa kutokana na Kamistan kuwa na mpango wa kumiliki nuclear(kama ilivyokuwa kwa Iran); hatimae ni President Hassan mwenyewe (wa Kamistan) ndie aliamua kuachana na mpango wa nuclear kama ilivyotokea sasa kwa Rais wa Iran.
- President Taylor wa US (wa series 24) alihakikisha kwamba mpango wa President wa Omar usisimamiwe na US bali UN, kama inavyotkea sasa…kwamba ingawaje mdau mkuu wa uhasama wa kinyukilia kati ya US na Iran ni US lakini US ameacha mpango huo usimamiwe na UN!
Kwa bahati mbaya sana, Rais Omar Hassan wa Kamistan hakufikia malengo yake ya ku-sign peace agreement deal baada ya hardliners kutoka nchini mwake, wakisaidiwa na Urusi kuhujumu mpango huo. Hatimae, Rais Omari aliuawa na hao hardliners baada ya kunusurika shambulio la kwanza ambalo lilikuwa coordinated na mdogo wake Farhad!
Rais wa sasa wa Iran, Hassan Rouhan hajapata misuko misuko sana kutoka kwa hardliners wa Iran ambao kimsingi wana nguvu sana kwenye siasa za nchi hiyo. Hata hivyo, si kwamba yupo salama sana coz' hata wanamageuzi wenzake wameshaanza kuhofu kwamba jinsi vile alivyo-concetrate kwenye kurudisha uhusiano mwema na Mataifa ya Magharibi, inaweza kumpunguzia imani kwenye siasa za nyumbani. Aidha, hata hardliners wameanza kutoa criticism za hapa na pale…ikumbukwe kwamba, mafanikio ya ya President Hassan Rouhan kufikia nia yake itategema sana full support ya Supreme Leader, Ayatollah Ali Khamenei. Supreme Leader ndie mwenye maguvu kwa siasa za Iran lakini kwa bahati mbaya sana huyu uzungukwa na military hardliners na conservatives. Ingawaje Ayatollah Ali Khamenei amemwachia uwanja Hassan Rouan linapokuja suala la kushughulikia Nuclear issues lakini upinzani ambao Rouhan aliupata hivi karibuni watu wanatafsiri kwamba hata kama ameachiwa uwanja, bado analazimika kupata go ahead kutoka kwa Khamenei!
All in all, will President Hassan Rouhan of Iran make it or end like President Omari Hassan of Kamistan? Will he get another chance in the coming election (2017) au atakumbana na mizengwe kama ambayo alikumbana nayo mwanamageuzi mwenzake President David Palmer (24 Season I-III)?