Tutunze mazingira yetu

idiomer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2012
Posts
238
Reaction score
258
Mazingira Mazingira Mazingira
Mazingira safi ni muhimu kwa viumbe hai.

Jukumu la kutunza mazingira ni la kila mmoja wetu. Pia ni jambo la hiari sio la kutumia nguvu.

Mwandishi mmoja wa kitabu cha "How to get whatever you want (M.R. Kopmeyer)

Anatuasa kama tunataka matokeo chanya tusitumie nguvu. ( Pressure create resistance and force create enemies)

Kusema mtu akitupa ganda la ndizi au pipi kwa mkoa wa Dar es salaam atalipa faini ya milioni 1 imekaa kinguvu sana.

Nafikiri kuna NGOs nyingi za mazingira Mkuu wa u wa mkoa angeweza kuwaita na kuona jinsi gani wanachangia kwenye kuweka mji safi. Pia kuna watu wa NemcTanzania ambao wanaweza kukumbusha watu katika kanuni na sheria mbalimbali za kutunza mazingira.

Pia ukiangalia Jiji la Dar es Salaam watu ni wengi na wanaendelea kuwa wengi hivyo ni vema pia mahitaji kama sehemu za kuweka taka kwa muda ( dustbin πŸ—‘) kuwekwa sehemu za vituo vya mabasi kama mbezi, mawasiliano, Mbagala, Posta , Mwenge na sehemu nyingine zenye msongamano wa watu.

Kila nyumba kuwa na πŸ—‘ ni jambo zuri sana.
Ila kwa kuanza na taasisi zote ambazo zinakuwa na watu wengi pia ni muhimu kuwa mifumo ya kuteketeza taka kama incinerator, au mifumo ya mashimo kuchoma taka.

Pia daladala abiria lazima wawe na dustbin ndani wanaweza kuzalisha takataka kwa kununua vitu pindi wakiwa safari fupi.

Elimu Elimu Elimu
Elimu ya mazingira iendelee kutolewa kuanzia mashuleni. Watu wote tunapitia shuleni hivyo club za mazingira ziimarishwe na matangazo yawe mengi kulinda mazingira.

Kila mfanyabiashara awe na dustbin. Biashara ka za wauza vyakula na vinywaji zinazalisha taka nyingi sana. Hivyo kundi hili liwe na dustbin πŸ—‘.

Pia mwisho pawe na mashindano ya usafi ya wilaya za jiji la Dar es Salaam. Kigamboni, Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo. Hii italeta chachu na kumpunguzia mkuu wa mkoa kazi kubwa.

Uzalendo unaanza na kutunza mazingira ili kuzuia maambukizi ya magonjwa, mafuriko, afya ya akili
(Sehemu kuwa na kelele nyingi), utulivu wa kujisomea kwa wanafunzi.

Maoni ya Mwalimu

Kwako mkuu wa mkoa
Albert Chalamila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…