Tushauriane wote

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,146
Reaction score
7,685
Ni ndefu lakini acha uvivu soma itakusaidia sana.

" Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda.

Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati.

Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba. Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake.

Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo.Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake.

Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake.

Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho.Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana.

Kijana akaamka na kutoa mfuko, kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate, watu wote wakastaajabu.

Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia. Akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha.

Akiwa analia akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.

Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota. Kisha akarudi high table na kusema "baby nakushukuru kwa yote. Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii.

Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya.." Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday.

Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema "Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa.

Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.

Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza.." Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late.

MORAL OF THE STORY

Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida. Kuna vingi vya thamani ndani yako. Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima.

TUELIMISHANE MEMA Usisahau kucha comment ako ni muhimu ili tuelimishane na tupeane njia za kutambua yupi ni wa kweli na yupi muongo.
 
sina coment nzuri lakin inaonyesha huyo dada hakua na ule upendo wa dhati
 
Eee si dada zetu wa dotcom hao bila zawadi ya gari besidei ainogeki big up kwenu
 
Smtym.mapenz hayahitaji akili nyingi...mambo ya kuweka vitu muhimu kwene mikate vya nn....we mpe tu bas....ona sasa kamkosa mtoto mang'anyuuu
 
Smtym.mapenz hayahitaji akili nyingi...mambo ya kuweka vitu muhimu kwene mikate vya nn....we mpe tu bas....ona sasa kamkosa mtoto mang'anyuuu

Ukiwafanyia hao hvyooo utalia kaka labda kama mwenzetu una nyota ya chips mayai
 
sina coment nzuri lakin inaonyesha huyo dada hakua na ule upendo wa dhati

Nw dayz wa dada wanaopenda kwa dhati ni mmoja kwa kumii wengi wapo kipesaa......mke una lala nae sa nne usiku anakuomba hela una mwambia sina kabisa...mnalala wote asubuhi sa moja mna amka wote anasema naomba hela sa sijui anajua usiku ulitoroka kwenda tafuta
 
Ukiwafanyia hao hvyooo utalia kaka labda kama mwenzetu una nyota ya chips mayai

Kuamua kutoa zawad ni sawa na kutoa sadaka....so ye kama atakuona ndezi poa tu ila we umetoa zawadi....as long as papuch lake nalitumia shaka sina
 
Great! Hapa ndipo wanawake wapenda pesa, wanapofanya hesabu za 50-50
!!
^^
 
Eee si dada zetu wa dotcom hao bila zawadi ya gari besidei ainogeki big up kwenu

Ni shidaaaaa dada zetu hawa wanapenda mwanaume mwenye gari akati hata baba ake hana gari sasa sijui wanashindwa kuiga mfano wa mama zao
 
Kuamua kutoa zawad ni sawa na kutoa sadaka....so ye kama atakuona ndezi poa tu ila we umetoa zawadi....as long as papuch lake nalitumia shaka sina

Hahahahaha akikutenda hata hilo papu utaliona la motooo
 
Hahahahaha akikutenda hata hilo papu utaliona la motooo

Mkuu nmejaliwa moyo mgumu sana....nina ugonjwa uwa siamin.mwanamke...so akibadilika nshajiandaa kisycolojia....ila papuch lake uwa nalitumia effectvely
 
Reactions: 7ve
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…