Nakumbuka mwaka 2016 nikitokea maswa kwenda jijini mwanza, tulipofika buhongwa basi ikapigwa mkasi na karandinga wakashuka washikaji wawili wakamfiata mdau niliekuwa nae siti moja wakampiga bangili..... Mshikaji akasema Mimi ni asikari huku anataka kulia huku analeta ubishi kuvaa bangili. Alipoonyeshwa mguu wa rungu alinywea tuliii,
Alipofikishwa mlangoni mama mmoja( nadhani alikiwa anamsaka mtuhumiwa) akasema sio yeye!
Wakati wa sakata jamaa mmoja akaruka dirishani akatimua mbio ambaye ndiye mtuhumiwa og!
Poti akafunguliwa pingu akaanza kufoka sana, washikaji zake wakamwambia potezea.... ukijichanganya kwa matusi tena jioni RPC atasoma press!
Akawa mpole saaana, had I lnyegezi haongei.
Nakuunga mkono, hata polisi mwenyewe likimtimbia karandika wapo full helment atapaniki vibaya mno