Musoma Yetu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2016
- 2,635
- 2,303
Jamani watanzania, nchi hii ilikuwa shamba la bibi kwa kipindi kirefu. Tunaiomba serikali ya awamu ya tano, kwa nguvu iliyoelekeza kwenye watumishi wa umma, vile vile itumike kupitia upya hii mikataba ya madini na gesi , ikiwemo ile sheria ya muswada wa madini na gesi iliyopitishwa bungeni.
Mkuuuu nakusikitikia kukuambia usahau.hayo unayoaandika kutokeaTena Raisi afanye haraka sana ili tujue nini kinaendelea kwenye makampuni yanayochimba dhahabu na Almasi mfano GGM, ACACIA, MWADUI, TANZANITE ONE, CATA MINE, na mengine mengi. Pia sheria ya gase na madini ipitiwe upya kabisa. Pia yale maazimio ya bunge ya mwaka jana juu ya IPTL pia yale matrioni ya USWISI yalejeshwe ili tufidie pengo la MCC. Serikali ifanye haraka sana kutafuta wadau watakoanza uchimbaji wa gase mpya iliyogunduliwa hivi karibu ili ianze kuuza nchi za nje na hivyo kuweza kupata fedha za kigeni na kuiimalisa shilingi yetu.
Lakini unafahamu vyema sheria za kimataifa za mikataba? jee hio mikataba inaruhusu hicho kipengele cha kuipitia upya maana kuna mikataba imejifunga kwa zaidi ya miaka 100. Kusema ni rahisi kuliko kutenda. Kuhusu mikataba basi Muulize Cuba na issue ya Guantanamo Bay!
nadhani tungeanzia na kuweka migodi iliyobinafsishwa na mwaka ambao serikali ilitiliana hiyo mikataba na wawekezaji.,Jamani watanzania, nchi hii ilikuwa shamba la bibi kwa kipindi kirefu. Tunaiomba serikali ya awamu ya tano, kwa nguvu iliyoelekeza kwenye watumishi wa umma, vile vile itumike kupitia upya hii mikataba ya madini na gesi , ikiwemo ile sheria ya muswada wa madini na gesi iliyopitishwa bungeni.
tumia japo sehemu ya muda wako kidogo kuitafutia ukweli na sio kulewa mbege tu na kuja kutapika humu.Hapo Mkwere alishamaliza kazi yuko anakula ten percent yake hadi wajukuu...