kama ukisikia dhuluma ni hii ya wastaafu kupunjwa hela zao eti wataathirika mitaani wakipewa zote. Na eti wanawahi kuishiwa na kubaki wakiishi maisha ya chini. Kwanza ifahamike kiwa hii serikali haitaki kuwajali watumishi wake. Tangu mwaka 2015 ni watumishi wachache sana wamepandishwa vyeo na nyongeza ya mishahara hakuna. Kwahiyo mtumishi kama walivyo watu wengine inabidi achukue mikopo na kuishi kwa kipato cha chini sana. Hapa analazimika kupunguza baadhi ya matumizi zikiwema huduma za lishe bora. Baada ya kustaafu inabidi apumzike na kuanza kula matunda ya kazi yake
Cha ajabu anapokumbana na mafao yasiyoridhisha ndoto yake lazima afya yake itayumba. Hii 35% ni hela ndogo sana isiyotosheleza chochote kwa mstaafu. Ni iweje serikali iwe na maamuzi mabaya namna hii. Kuna nini nyuma ya pazia? Je nini utetezi wa vyama vya wafanyakazi juu ya hili. Ni kwa nini hatuwasikia wabunge wakitetea jambo hili. Ni vipi huyu mstaafu na yeye akaanzisha miradi yake na kujihesabu kuwa muwekezaji au hata kuanzisha mradi wa kilimo. Hivi ni kwa nini rais adilitolee maamuzi kama alivyofanya kwenye bei ya klrosho. Au huyu mstaafu anafanyiwa hivi kwa sababu halindi kura na pengine idadi yao ni ndogo.
Tufike sehemu tusianze kuchezeana kwenye mapato. Mfano kwa mtu uliyetumika serikalini kwa miaka 40 na kuwa na akiba ya milioni 100 halafu unakuja kuambulia milioni 35. Hii naona si sawa, fedha zinapungua thamani mfano leo thamani ya dola haitolingana na thamani ya dola miaka 12 ijayo. Na lek hii nikichukua milioni 100 zangu nikatengeneza miradi, baada ya kipindi nitakuwa mbali sana. Jamani hawa wabunge wametutia umasikini bila sababu. Hivi juhudi zipi za serikali ambazo zinawatoa wabunge upinzani kwenda kuziunga kama hali ndiyo hii. Iweje mtu mkamilifu aende kuunga juhudi kuwatia wenzake umasikini. Hela za mbunge miaka 5 haiguswi na wanapata zaidi ya milioni 200. Sisi wastaafu tunapewa chini ya mia. Naomba rais Maghfuli alione hili