Hayo siyo maamuzi ya Lissu bali ni ya chama.
vipi yule dada aliyesaidia kumuandalia mkutano pale serena ameshaipata hii taarifa??
Nimetonywa anaitwa shonzy....
Pokea pongezi zangu , umeandika kikakamavu sana !
8.0. HATUA ZA KINIDHAMU KWA WABUNGE, MADIWANI,WENYEVITI WA VIJIJI/MITAA NA VITONGOJITuwekeeni kifungu hicho cha katiba ya CHADEMA kinachosema hivyo?!
Mbona mnaongea hewani hewani tu?!
Sasa hivi hawana nguvu sana ya kumtetea kwani huko kwao kunawaka mioto! ACT wanapigana vikumbo, CCM wanapigana vikumbo. ZZK ataenda kufundisha uchumi kama alivyowahi kuahidi huko nyuma!
8.0. HATUA ZA KINIDHAMU KWA WABUNGE, MADIWANI,WENYEVITI WA VIJIJI/MITAA NA VITONGOJIHivi mkuu wewe unaweza kuomba msamaha wakati huna kosa? Au kosa lake kuonyesha nia ya kumtoa dikteta MBOOwe? Hadi pale alipoambiwa kijana tumia busara? Ndio maana ya Demokrasia hiyo kwenye chama chenu?
Kumbe katiba mnafuata baadhi ya vipengele tu? Vipi uwepo wa m/kiti wa sasa hivi ndugu Dj MBOOwe kuongoza kwa muhula wa 3 huu? Huoni mpkm anaenda kinyume na katiba aliyoiapa kuwa atailinda na kuitetea? Tatizo lenu CHAGGADEMA mnaongozwa kwa hisia na HISIA na VISASI na si lolote lile.
..but necessary as per their constitution.......
Very Good..Na imekuja ktk right time...arudi tena mahakamani.Ili akamaliziwe kabisa kisiasa.CCM na Bunge lao ndio wajiulize km ilikuwa worth kumpati kamati na kumpa jukwaa kiasi hicho.Mwanasheria mkuu wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama kwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe. "Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa CHADEMA. View attachment 233406
Zitto anatoa mchango mkubwa sana Bungeni, na mara zote anaibua hoja nzito zinazokuja kusaidia japo kujua wizi unaofanyika, cdm kama chama kingemshauri na kumrudisha kundini aendelee kuitumikia nchi, hii timua timua haisaidii lolote...
Hasante kwa bandiko hili ndugu, isipokuwa hapo kwenye kumfukuza naona wako sahihiYeah, Zito amepoteza kabisa trust ya CHADEMA. Lakini mimi napoifikiria zaidi nchi nahuzunika sana kwa uthibitisho unaozidi kujitokeza kwamba mahakama zetu ni za ovyo kabisa (kangaroo courts). Yaani siasa za kifisadi ndizo zinazoendesha mahakama; just like the Italian or Russian mafia! Zito alipewa kinga kubaki CHADEMA walipopenda "wenyewe". Leo hii kawaudhi, kinga inaondolewa chapchap, kisa?, amepoteza umuhimu! Ndugu zangu CHADEMA mngelifikiria hilo kwanza, msingepoteza muda kujitokeza kutangaza rasmi kumvua uanachama Zito; mngemuacha tu adondoke mwenyewe taratibu kwa kanuni zilizopo. Hii Tundu Lissu kujitokeza kutangaza, ni kama kuipa mahakama hadhi isiyostahili kabisa. Msipofushwe na kero moja pekee. Mngechukulia kwamba wote: Zito na mahakama ni uozo mtupu. Huo uamuzi wa mahakama umetolewa katika mazingira ya ovyo sana; si kitu ch kujivunia wala kuchangamkiwa na chama kama CHADEMA.
Pamoja na kwamba nilikuwa nafurahishwa na uwezo na ujasiri wa Zito katika kujituma kufuatilia mambo muhimu ya taifa, hivi leo sijali sana kama kapata shule au la kwani nimeona baadhi ya binadamu, kwa namna ya kushangaza sana, wako tayari kuchezewa na wahuni - bila sababu za msingi. Mfano wangu best ni mama Tibaijuka. Mtu una karama bora kabisa; kazi zako za halali zinakupa kipato cha kujidai lakini unaamua kuwaachia "watoto wa mjini" wakupapase na kukupeleka arijojo kwa ujira wa ziada wenye kamba na idhara kibao. Inaniwia vigumu sana kuelewa kwa nini mtu awe hivyo?
kumbe zitto alikua ukawa?leo mmechanganyikiwa walah!
CHADEMA kwisha wacha wafu wawazike wafu wake sitaki tena kusikia chadema nimekua disappointed sana