Kumekuwa na tabia ya wanasiasa walioko kwenye nafasi zao kama mawaziri kufanya mabadiliko yasioyokuwa na kichwa wala miguu kwenye tasnia muhimu kama elimu bila kuwashirikisha wadau au kujali madhara yake, mfano wa mabadiliko hayo ni:-
1. Kubadili mihula ya A- Level kama homa za vipindi
2. Kuondoa michezo mashuleni
3. Kufuta masomo ya Kilimo, ufundi, sanaa, biashara
4. Kuunganisha somo la kemia na fizikia
5. Kuondoa hadhi ya mtihani wa kidato cha pili
6. Kupeleka walimu wakasome mwezi mmoja wakafundishe
7. Kubadili mitaala kila mara
8. Kuidhinisha vitabu visokuwa na kiwango vitumike shuleni
n.k
Mshangao wangu ni kuwa wanavyofanya maamuzi ya namna hiyo ambayo hayahitaji sana utafiti wa kina kuyajua yalivyokuwa ya kihuni wadau na wananchi wanakaa kimya kama haliwahusu
Najiuliza
1. Huwa wanatumwa na nani na kwa manufaa ya nani?
2. Wanaoathirika na maamuzi hayo wanafidiwaje?
3.Tutakaa kimya hadi lini?
Mkuu Lyamungo
Hatuna viongozi tunawachumia tumbo kiasi kwamba yeyote anapoamua wengine nao hupitisha kwa
upumbavu ndiyooo bila kutafakali wala kutathimini athali za mabadiliko ya mara kwa mara kwa Vizazi vya watanzania na Taifa kwa ujumala.
Suala la
elimu limegeuka kitendawili tangu baba wa Taifa aondoke madarakani, hatujapata tena kichwa cha uhakika katika kuwekeza. Enzi za mwalimu ilikuwa jambo la kawaida kabisa watoto wa mawaziliri na wakuu wengine wa serikali kusoma shule moja na
watoto wa walalahoi kutoka vijijini. Elimu ya matabaka haikuwepo.
Enzi za mwalimu japo shule zilikuwa chache
heshima ya elimu ya mtanzania ilikuwa juu, ubora wa elimu na uadilifu wa serikali kwa watanzania kuhusu elimu ulikuwa juu sana, walimu walithaminiwa na vifaa vya kufundishia vilipatikana.
Enzi za mwalimu hapakuwa na
elimu ya matabaka kama tunavyoshuhudia hivi sasa, shule za kata moja kwa moja zinaandaa mazingira ya
watoto wa wakulima kutawaliwa na
aKina malecela, Riziwani na ndugu zake, makamba, mwinyi nk.
Usitegemee kabisa kuwa na elimu bora unapokuwana
Raisi kilaza kama kikwete anaye tukana walimu waziwazi, mishahara mibovu, kuiongeza hataki na kwa kejeli akitumia mahakama kuwakandamiza. (Wakenya wanafahamu kwamba
kuchezea elimu ni upumbavu wamejadili na kufikia muafaka na walium)
Tanzania itabakia kuwa taifa la mbumbumbu kwa muda mrefu kwasababu
damu za watawala walewale wenye fikra mgando zinaendelea kututawala unless aina ya watawala wengine wenye uchungu na Taifa tanzania wakaingia madarakani. (kama ilivyo katika michezo na laana yetu ya kichwa cha mwendawazimu)
Unapoona wanasiasa bungeni wakisifu kwa
idadi ya wingi shule na wanafunzi bila kujali ubora wa elimu itolewayo na ubora wa wahitimu hakika Taifa limepotea njia na kuirudia njia sahihi itahitaji
kichwa kingine chenye maono ya kweli katika kumkomboa mtanzania.