Tumpeni ushauri afanye nini?

KUWEDA

Member
Joined
Mar 5, 2013
Posts
41
Reaction score
6
Habari zenu wana JF!?...nina jamaa yangu niliyesoma nae enzi hzo,tulitengana muda wa miaka kama saba hiv,lakin tulikua tukiwasiliana kama kawaida.
Hivi juzi kanipigia cm anaomba nimshauri juu ya jambo lifuatalo:
Anadai amefikia umri wa kuoa nae ni miongon mwa watu wa jamii za wafugaji,hvyo anatarajia kuoa mwezi wa6 mwaka huu,mchumba yupo tayari kwa kuolewa kilichobaki ni mahari(ameambiwa apeleke ng'ombe 60)baba yake amekubali kumtolea hao ng'ombe 60 ila kwa sharti la kutomsaidia kngne zaid yeye msaada wake ni huo..jamaa nae ni mkulima wa kawaida anamiliki nyumba ya nyasi yenye vyumba viwili na ukumbi 1..sasa jamaa anachoniuliza mm nimshauri ni kuwa yy ataka atoroke na hao ng'ombe pindi atakapokabidhiwa,wakati huohuo anataka kumtorosha pia mchumbake...SWALI ALILONIULIZA;"NIWAPELEKE HAO NG'OMBE AU NISEPE NAO?"nipeni mawazo yenu nimjibu.
 
hahahaha nacheka kama mazuri lakini huyo hatumii akili anataka pande zote aharibu hakumbuki kuwa hii dunia ni mzunguko kuna leo na kesho anaweza kupata tatizo atakimbilia wapi kuomba msaada,nahisi kwa sasa bado niko kwenye bumbuwazi ngoja niishie hapa.
 
Kwani kwanini anataka kufanya hivyo?

Mi sijaelewa, utajiri anataka au? Atatoroka na ng'ombe 60 hadi wapi anadhani? Ataenda kuishi kwenye sayari nyingine? Hajui kama atakuwa amegombana na ndugu na jamaa wa ukoo zote mbili? Anataka kumuharibia dada wa watu bure kabisa

Si anapewa bure hao ng'ombe na baba yake, kama anataka wa kwake si aanze ufugaji na yeye.

Nadhani umri wake wa kuoa bado, hajakua huyo bado asubiri kwanza akue.
 
Yaani uzi ni komed mwanzo mwisho...ila kuoa kwa ng'ombe 60 na wakat huna uhakika na maisha...ni kujichapa viboko mwenyewe....mwambie amuombe baba yake hzo ng'ombe hasepe nazo akajipange upya...ng'ombe 60? Mmja ni zaid ya lak 5
 
hii story ni ya kweli?

Unaishi nyumba ya nyasi na una ng'ombe 60(of course kwa sasa bado ni ng'ombe wa baba) si heri auze ng'ombe afanye biashara?????
 
aombe hao ng'ombe 60 thn akipewa kihalali na baba yake naamin akiwa2nz vizur kwa miaka michache wanawez fika 100..kuoa kupo 2 japo mke anawez asimsubiri..
 
Ng`ombe 60, how come, wapi huko.

Duh kwa mtaji huu nakosa imani kama mateso, manyanyaso, utumikishwaji kwa wanawake vitakwisha, huyu binti ni kama atakuwa ameuzwa vile.
 
Naona dalili kama kastory ka kusadikika hivi.. NWY, ngoja wenye taaluma za kuchakachua wanakuja kukupa mbinu
 
BADILI TABIA kwa jamii za wafugaji ni kawaida sana! Lakini kinacho nishangaza huyo jamaa mbona kama elimu haijamkomboa kabisa? Maana kama wana ng'ombe zaidi ya 60 kwa nini aishi hivyo?
Pengine hata baba yake anaishi nyumba ya namna hiyo!
hii story ni ya kweli?

Unaishi nyumba ya nyasi na una ng'ombe 60(of course kwa sasa bado ni ng'ombe wa baba) si heri auze ng'ombe afanye biashara?????
 
Last edited by a moderator:
Mbona jibu linaonekana wazi hapo! Ng'ombe 60 mnabadilishana na duka la spea za magari au?!
 
Achukue ng'ombe, amuache binti. Akafanye biashara miaka 2; arudi akatoe hao ng'ombe 60.
 
Hapa mtamponda huyo kijana lakini hiyo ndio akili.
Huwezi kutoa mahari ya ng'ombe wote hao halafu uendelee kuishi maisha ya dhiki.
Kama kweli haya yanafanyika Tanzania basi sisi ni moja kati ya mataifa ya watu vilaza.
Kuweza kutoa ng'ombe wote hao maana yake ni kwamba huyo mzee anao ng'ombe zaidi ya hao na bado ni maskini(moyoni kwake anajiaminisha kuwa yeye yu tajiri kwa kuwa tu ana ng'ombe wengi kama utitiri).
 
samahani JF, Naomba mniruhusu kucheka! hahahahahahahahahaha! Mambo ya kwetu usukumani bana duuuh!
 
samahani JF, Naomba mniruhusu kucheka! hahahahahahahahahaha! Mambo ya kwetu usukumani bana duuuh!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…