Hakuna lolote tulilojifunza kwa sababu yote yale ambayo watu tumekuwa tukiyazungumzia miaka nenda rudi yametokea. Na tushukuru kuwa hili janga la mafuriko si la maangamizi makubwa kulinganisha na tuseme Tsunami au tetemeko kubwa la ardhi nchi kavu. Haya mawili na yatupitilie mbali la sivyo tutafutika kabisa katika ramani ya dunia.
Kwa ujumla hatuko tayari kukabiliana na majanga, serikali yetu haijitambui wala kujielewa ipo madarakani kwa madhumuni gani, vipaumbele vyetu havieleweki (wametumia mabilioni kusherehekea Uhuru wakati mambo muhimu yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja wameyatelekeza), baada ya muda na sisi wananchi wa kawaida tutasahau kila kitu, na ifikapo mwaka 2015 tutazidi kuwachagua watu wale wale watuongoze tena.