Sijui nilikuwa natafuta nini kwenye begi la sister ebanaee si nikakutana na ka kadi hivi kazuri kufungua nikaona makopa na mishale kwa pembeni kimeandikwa kwa mkono nikasoma kuona nikang'amua sista anatongozwa tena vesi deadly, nikaona hiki ki kadi kitanifaa nakapita nacho.
Nikatoka home nikaenda mlimani kukisoma vizuri ili nipate utulivu na nisionwe pia(mwanza kuna milima sana)
Yaani kile ki kadi nilikielewa sana yule mwamba alishuka stanza tena alichonifurahisha hakuandika jina la sista wala jina lake nikacheka kichizi maana ile kadi nikaona inanifaa tena ntaipeleka kwa dem nliokuwa namtaka ila nlikuwa sijui pa kuanzia.
Kipindi iko nilikuwa darasa la 5 kama kawaida mapumziko nikampelekea Naomi yeye alikuwa darasa la sita halafu mzuri shule nzima.
Huyu naomi alikuwa dada mkuu, msafi na mimi nilikiwa nang'aa maana sista alikuwa hataki nipauke kiboya maana mi kufua ilikuwa mpaka siku ya usafi, sista anafua kila siku akawa ananifulia nakuninyooshea dogo lake ning'ae sista alikuwa sekondari, kwahiyo kipindi napeleka kile kikadi kwa naomi nilikuwa nang'aa tunaendana usafi ila mi ni dogo naomi ananizidi darasa na umri.
Naomi akapokea kile kikadi akaniuliza nani kakupa nikamuambia mimi ndo nimekuandikia huo ujumbe tene imebidi niulete mwenyewe ili nihakikishe umefika na umeupokea.
Naomi akaniangalia afu ananiambia toka urefuke kama mpapai unawafuata hadi dada zako. Nikamjibu kwa nidhamu "ungeenda ukasoma kwanza yaliyomo ukayajua halafu ndo utajua kama ulivonambia narefuka kama mpapai ni sahihi au sio sahihi"
Naomi akasepa, nadhani hakujua kile ki kadi kimetoka sekondari maana yule mwamba aliyeandika saivi ukute ni docta love labda, naona Naomi alivosoma huko akakutana na stanza kuntu akaelewa.
Sasa shida ikaja ni mimi kifuata jibu maana nilianza kumuogopa dada mkuu ukizingatia alikuwa ananizidi darasa na miaka miwli plus lile biti alilonipiga.
Ukapita mwezi mimi sijamfata tena Naomi maana nilikuwa namchenga ebanae si akaniandikia barua ya kunikubali akatuma mtu aniletee.
Hiyo barua ya kukubaliwa niliisoma kila nilipokuwa pekeangu, kwanzanlikua natoka home naenda mlimani kuisoma kila siku utadhani sijawahi kuisoma hapo nyuma.
Naomi akaingia lasaba mi darasa lasita ni dem wangu ila nilikuwa namuogopa kishenzi maana nilikuwa sijazoea halafu nilikuwa sijawahi, halafu hata sijui cha kufanya wala. Nakumbuka kuna siku alinikumbatia ilikuwa jioni karibu na kwao alinibusu shavuni na mimi nikamshika kiuno na kabusu kangu huku naogopa ila nlijikaza, sikuhiyo nadhani ndo siku nliokuwa na furaha duniani nilirudi home usiku sikulala.
Sista wangu alikuwa anapenda kufua nguo zangu za zule akiwa nanafua zake halafu ananyoosha ili shuleni nig'ae maana mi ilikuwa kufua mpaka siku ya usafi.
siku anafua si akaiona ila barua ya Naomi ilikiwa kwenye kaptura maana nlikuwa natembea nayo ili nikipata gepu la kuisoma naishoma halafu nafurahi kishenzi maana naomi ni pini alikuwa na curvy falani ivi deadly, lips dende ila nlikuwa sijui kuzitendea haki, tako kama kawaida iyo ni pie(π), macho akiniangalia sijiwezi, mguu shampeini sio fanta passion
Sista akaiona barua Naomi ananikibalia halafu alijiandika na jina mule na mimi akanitaja eti nampotezea maana hata simtafuti.
Sista alimjua naomi kwa sababu alikuwa dada mkuu halafu naule uzuri kila mtu alikuwa anamjua.
Sista alishangaa mimi kuwa na dem pini vile wakati ananionaga fala, akaniuliza nimempataje Yule Dada mkuu nikamuambia yule mbona ni dem wangu toka nipo Darasa la tano mwishoni.
Sista akaniuliza umesha piga? Nikashindwa kujibu akajua bado akaanza kunipanga mwambie naomi aje,,,
Nikaanza kufuata maelekezo ya sista. Maana kabla ya hapo ilikuwa kukitana na naomi mpaka njiani tu lalafu from no where au niende kujipitisha karibu na kwao tena bila appointment.
Naomi anakuja nakaa nae hata sifanyi chochote badae namsindikiza nikirudi sista anani mindi yaani ukweli juhudi za sista ndo zilinifanya nipige tena baada ya miezi saba. nashukuru sista aliiona ile barua maana bila hivo nilikuwa nimejishkisha pembe.
Nimechoka kuandika hata ivo huu sio uzi wangu.