Tujadili homa ya Uti wa Mgongo(Meningitis)

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Nimeangalia chombo kimoja cha habari leo kati ya habari zao leo ni Vifo vya watu 200 kutoka Nigeria vikiwa vimesababishwa na Homa ya uti wa mgongo(meningitis)

Meningitis ni Ugonjwa unaoshambulia leya inayolinda ubongo na Uti wa mgongo(meninges).

Ugonjwa huu huweza sababishwa na Bacteria,Fangasi na pia Virusi ila Asilimia kubwa ni Bacteria.

Ugonjwa huu ni hatari sana kwani hushambulia Ubongo Ambao ndio Injini katika mfumo wote wa Fahamu

Dalili zake ni kama vile maumivu ya kichwa,homa kali,viungo/misuli kukakamaa(muscle stiffness) kutapika,kizunguzungu,kuishiwa nguvu...nk

Kama kujua mgonjwa anaugonjwa huu kinafanyika kipimo cha Lumbar puncture na kuchukua celebrospinal fluid na kwenda kupima.

Kwa kifupi sana ndo maelezo juu ya homa ya uti wa mgongo(meningitis)

Kitu cha kujiuliza kwanini Umeua kwa Kasi Nigeria sana wakati Kesi zake ni chache sana kwa mwaka unaeza usipate mgonjwa hata mmoja mwenye homa ya uti wa mgongo kwanini Umekuja kwa Kasi hivi?


Karibu tupeane shule zaidi juu ya ugonjwa huu
 
Mkuu nadhani ulisoma EPIDEMIOLOGY,

Ukanda wa Afrika magharibi, Afrika ya kati mpaka ASIA inasadikika kuwa kuna bacyeria wengi (Neiseria species) hasa hasa Neiseria meningitidis ambao husababisha meningitis,
Ugonjwa huu huua maelfu ya watu kwa mwaka huko afrika ya magharibi ikiwemo nchi ya Nigeria
 
There must be risk/predisposing factor!..hii inategemea pia na age group....kwenye maelezo yako hujaelekeza ni group gani la umri ndio waathirika zaidi!..
Low immunity
autoimmune
hiv infection.
Alcoholism
Spleen removal
Bacterial endemic kama mdau mmoja alivyosema hapo juu kuwa hayo maeneo yana Neisseria meningitis bacteria infection.
 
Back
Top Bottom