Nianze kwa kusema, hata ikulu kuna wasaliti, vibaraka na watu wasio waaminifu!Si ndio maana hata vikao vya ndani(siri) taarifa zake zinasikika baada ya kikao?!
Nadhani, kule kuchoshwa na utawala uliopo kuliwafanya/kunawafanya watu kupenda chama bila matarajio. Yaani, kuamini hakutakuwa na msukosuko siku zote ndani ya chama, kutakuwa na ustawi mzuri wa chama daima, Hapa walikosea/wanakosea.
Ni kweli, kuna matarajio fulani(makubwa kiuhalisia) kutoka kwa watu kuelekea chama cha CHADEMA, lakini nadhani matarijio haya yangeenda sambamba na mategemeo ya kupata misukosuko mbalimbali (makundi, vibaraka, kutoaminiana, tamaa n.k)
Umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu. Niaminivyo mimi, kuna watu fulani wanavutiwa sana na utendaji kazi wa mtu fulani ndani ya CHADEMA mf. Dr. Slaa W.P, au Mh. Zitto Z Kabwe, au Mh. Tundu Lissu, Mh. F. Mbowe n.k. iwapo kutatokea kuondoka kwa mmoja wa hao(sio niliowataja tu,ilikuwa mfano), kunaleta upungufu wa imani(matarajio), wafuasi n.
Haijalishi, atakayesimana katika kugombea urais ni nani(IWAPO TU, lengo ni kuwatetea wananchi), maana watatekeleza na kusimamia ilani ya chama(Regardless who stands) na pindi watakapokuwa madarakani watasimamia na kuwatetea wananchi wa taifa la TANZANIA na si wafuasi wa CHADEMA au vinginevyo.
Malumbano yanayoendelea hasa kwa hawa vijana, hayasaidii.Kujishusha wakati fulani ni muhimu katika maisha, michakato mbalimbali.
Hivyo, hebu rudini mwanzo, mlivyojiheshimu, mlivyofanya kazi kwa umahiri, angalieni upya imani mliyojenga, mafanikio mliyoyapata, sehemu kidogo iliyobaki kumalizia, na juhudi kidogo inayohitajika. If all that doesnt worthy it, go ahead with the drama.