Tuangalie Mapenzi

mussa bakari

Member
Joined
Sep 20, 2014
Posts
13
Reaction score
13
Tuangalie nini maana ya mapenzi

Mapenzi ni upendo wa dhati utokao moyoni
mwa mtu wala si kuvuliwa nguo na mtu . Sijui kama nimeeleweka hapo nina maana gani

Ngono si upendo bali upendo wa kweli upo
moyoni kwa mtu na siku zote apendaye ni
mvumilivu wala hatangulizi ngono mbele humjenga kwanza mtu moyoni ili awe tayari
kuishi naye kwa tabu na raha.

Najua wapo
wasiokubaliana nami kwa kuona bila ngono
hakuna mapenzi

Nikikuuliza swali , hivi wanaouza miili yao
wanawapenda wangapi? Jibu lazima utaona
wapo kwenye biashara , wala hawana mapenzi
na mtu . Kwa jibu hilo utajua ngono si penzi
kamili.

Nachukua fursa hii kuwasifu wasichana wote
wanaojua thamani ya miili yao , kuwajua
wanaume wasio wakweli wanaotanguliza
ngono mbele . Hao hawana mapenzi ya kweli
bali tamaa ya ngono ndiyo inayowasumbua ,
wakishaujua mwili wako mapenzi
yamekwisha.

Mwisho napenda kuwashauri wote wenye
mapenzi ya kweli wasitangulize ngono mbele
bali itakuja kwa sababu huyo ni mpenzi wako
kama kweli anakupenda haki yako ya ndoa
lazima atakupa kama hatakupa hapo una haki
ya kuona hakuna mapenzi. Asipokupa wewe
mpenzi wake , anampa nani ?

Siku zote mwenye mapenzi ya kweli humpa
mpenzi wake kile kilicho ndani ya uwezo wake
na furaha ya mapenzi ni kumfurahisha mpenzi
wako .

Nina imani kwa machache niliyoyasema kila
mtu atajua umuhimu wa kutanguliza upendo
ambao huzaa hicho unachokitaka.
 
Mwanaume alietulizana kidogo labda mwenye kibamia. Hawa wa vipaipu lo! Hadi kukojoa wanaelekezaga barabarani tuone.
 
Mwanaume alietulizana kidogo labda mwenye kibamia. Hawa wa vipaipu lo! Hadi kukojoa wanaelekezaga barabarani tuone.

Duh..Ngoja niongee kama Mzee Jangala "matushi hayo Mama Nshamu"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…