Trump apingwa dhidi ya ubaguzi

kwinyo

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2017
Posts
281
Reaction score
230
Umoja wa Mataifa umelaani kauli ya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyoitoa hivi karibuni kuhusu udhibiti wa wahamiaji weusi wanaoingia nchini humo kwaajili ya kutafuta maisha.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Msemaji wa Umoja wa Mataifa akizungumzia kauli hiyo aliyoitoa Rais Trump akiwa ofisini kwake,amesema[emoji117]kauli hiyo ni ya kushtua naya kibaguzi.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Rais Tump anadaiwa kuwa wakati akijadiliana na wabunge kuhusu mpango wahamiaji nchini humo alihoji[emoji117]Kwanini tunaruhusu watu hawa wote kutoka kwenye nchi alizoziita mashimo ya choo kuja hapa?.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Huku akizitaja nchi ya Haiti, El Salvador nan chi za Afrika.

Ikulu ya Marekani haijakanusha wala kusema chochote juu ya kauli hiyo.[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Katika wiki za hivi karibuni,Uongozi wa rais Trump umekuwa ukifanya jitihada za kujaribu kupunguza idadi ya familia za wahamiaji ambao watatakiwa kuingia Marekani,na tayari wameshawaondolea maelfu ya wahamiaji waliopo nchini humo.
 
Nimeisikia saa hivi redio ujerumani
 
Waafrika tunapenda mno kujishusha thamani mbele ya wazungu,,,, tukimuona mzungu kama tumeiona almasi 😀😀😀😀 mbona waarabu, wachina na pakistani hawako hivyo ndugu zangu.
 
Yaani alitaka kusema mndumku akatumia tafsida.
 
Njooni huku kwenu tupambane na haya madikteta yetu yanayoharibu taswira ya Afrika kimataifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…