Trilioni 1.27/- kukarabati vyuo vya polisi

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
SERIKALI imetenga jumla ya Sh trilioni 1 .27 kukarabati vyuo vitano vya polisi katika bajeti ya mwaka 2018/19, gharama hiyo ikijumuisha ukarabati wa majengo ya o si, mabweni, makazi ya wakufunzi na maeneo mengine yaliyoanza kuchakaa. Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea Chuo cha Polisi Kidatu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema hali ya miundombinu ya majengo kwa vyuo vyote ni chakavu, nia ya serikali na feshi la polisi ni kukarabati majengo hayo ili yaweze kukidhi mahitaji.

“Tuna vyuo vitano vya polisi nchini; Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo Dar es Salaam, Shule ya Polisi Moshi, Chuo cha Polisi Zanzibar, Chuo cha Maosa Kidatu na Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza hivi vyote vinahitaji ukarabati na tumetenga jumla ya Sh trilioni 1.2 kwa ajili ya ukarabati huo na tunamshukuru Rais Magufuli ameshatoa milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa chuo kimojawapo kati ya hivyo nilivyovitaja,” amesema Masauni.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho wajumbe wa kamati hiyo ya bunge waliitaka serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani kusimamia mafunzo yanayotolewa vyuoni humo, ikiwemo suala la wapelelezi kubambikia kesi wananchi, ikiwa ni kinyume na wachofundishwa vyuoni huku Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mussa Azzan Zungu akiitaka serikali kuwachukulia hatua askari polisi wachache wanaolichafua jeshi na kuivunjia heshima nchi kwa matendo yao ambayo
 
Wakarabati na elimu wanayotoa kwenye hivyo vyuo, mananga wengi sana siķu hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…