Ila unaambiwa ukiona foleni zinaongezeka mjini ujue ndio maendeleo yenyewe hayo. Kipindi cha nyuma miaka 70 hadi 90, tulikuwa tunatoka maeneo ya Mwembe Chai tunaenda Ferry kipindi hicho gari ni za kuhesabika, lakini sasa hivi maendeleo yamekuwa makubwa kiasi kwamba kwa vijana wa sasa gari wanaita BASIC NEED, yaani kama chakula, mavazi na malazi. Mtoto akimaliza chuo tu akipata kazi cha kwanza kabisa anakopa ili awe na gari, ni jambo zuri kwani ndio maendeleo hayo. Kibaya ni kwamba serikali imesahau kujenga miundo mbinu endelevu kulingana na ongezeko la watu jijini Dar na ongezeko la magari. Kingine kungefanyika mpango angalau wa kuiendeleza mikoa mingine nayo ili population ya Dar ipungue manake kha mpaka inakera. Watu wamekuwa wengi sana na kijografia huwa mji ni mdogo sana kuweza kubeba watu milioni 5 sijui (nasungumzia waliohesabiwa tu)