TRA na makusanyo ya kodi ya Majengo

namraroh

Senior Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
114
Reaction score
126
Baada ya mamlaka ya mapato kubaini kwamba idadi kubwa ya watanzania wameitikia mwito wa kulipa kodi ya majengo ni vizuri basi wakaendelea kuongeza muda ili kila mmoja wetu aweze kulipa kodi hiyo.

Kwa kuwa imethibitika kwamba wananchi wakihamasiahwa kulipa kodi wanatekeleza bila pingamizi ni vyema serikali ikawa na utaratibu wa kutoa elimu na hamasa kwa walipa kodi kwa ajili ya maendeleo yetu kwa ujumla.

Napenda kusisitiza kwamba endapo nguvu iliyotumika kwenye kuhamasisha ulipaji wa kodi hii ikitumika katika maeneo mengine ya ukusanyaji kodi, sisi kama taifa tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza utegemezi wa wafadhili katika miradi ya maendeleo na kulinda heshima ya taifa letu

Sent from my HM NOTE 1W using JamiiForums mobile app
 
Hakika mkuu wananchi wameitikia kwa hali na mali.TATIZO NI NAMNA MAFISI WA CCM WATAKAVYOZITAFUNA IZO PESA

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
kweli kabisa.nadhani na mm nilikuwa mmoja wao niliokuwa napinga TRA kukusanya kodi ila baada ya kuona walivyo hamasisha na kuweka sheria kali yulipanga msururu wenyewe na baada ya muda nikajua watanzania tukifuata sheria tutafika. safi sana though municipality nyingi zimekuwa hazina mapato sana ila nimefurahishwa ila wakazitumie vizuri kodi zetu kwa maendeleo ya wote hope tutaanza kulipa bila vitisho
 
Serikali ingeingia katika kupima viwanja na kuvipatia HATI YA MASHAMBA, MAKAZI, NA SEHEMU ZA BIASHARA wangepata Makusanyo makubwa sana na ingewekwa katika ASILIMIA
Kingine serikali inakosa Mapato makubwa sana kutokana kutoboresha biashara ya Kupangisha NYUMBA ZA BIASHARA, MAKAZI, NA MASHAMBA

Waamke na waachane na kukaaa Ofisini, na kusingizia Hakuna Budget
 
Hili ndilo tatizo kubwa la watumishi wa umma Tanzania, maadam wanalipwa mishahara yao basi hata kufikirisha bongo zao japo namna ya kuboresha na kuongeza mapato hawataki kufanya.
Ni muhimu kwa watumishi wa umma katika idara zinazozalisha mali na kukusanya mapato wakawa na malengo kuanzia ngazi ya mfanyakazi mmojammoja, kitengo, idara na hata mamlaka na kuwazawadia wanapovuka malengo hayo

Sent from my HM NOTE 1W using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…