jaribu kufuatilia kwa makini utagundua kuwa kila branch ya tra ina benki pembeni yake, nenda kilimanjaro pembeni kuna nmb na ndo wanaitumia kwa moshi, nenda morogoro mjini, pembeni kuna crdb na ndo inatambulika, nenda kinondoni(mwenge) pembeni kuna nmb na ndiyo inayotambulika kwa mwenge, nenda tra jknia(airport dar) malipo yote ya tra ya airport-dar yanafanyikia branch ya twiga iliyoko airport dar, pia ilala, tmk, na kwingineko kote utagundua kila penye tra kuna benki pembeni na inakulazimu kutumia tawi la benki lililopo karibu na hyo benki!
Je kwa nini inakuwa hvyo?
Unapojaza ile form ya kulipia tra huwa kuna copy ambayo benki inabaki nayo na nyingine tra orijino unabaki nayo mteja, ili tra wawe na uhakika kuwa umelipa unachotakiwa kulipa kuwapa ile copy ya malipo tu haitoshi, lazima watakwenda benki husika kuchukua nakala uliyoiacha huko wakati wa kufanya reconciliation. Sasa fikiria kila mtu amelipa katika benki yeyote ndani ya eneo husika huoni inawapa wakati mgumu kuanza kuchambua nani amelipia wapi?
Pia kila benki inayotumiwa na tra huwa imeunganishwa na tra kwa namna ambavyo tra wanaweza kuretrieve malipo yako bila kwenda physically benk uliyolipia.
Na kama upo makini utagundua si kila branch ya crdb iliyoko arusha unaweza kulipia tra!
Ni mawazo yangu tu, kama kuna watu wa tra huku watasema zaidi.