TPL na udhamini usioleweka!

africansongs

Member
Joined
Jan 5, 2018
Posts
83
Reaction score
225
Habarini wadau, ligi yetu nimeifuatilia kwa miaka kadhaa sasa na nilichogundua ni upuuzi wa hali ya juu unaoendelea huko.

Hasa hasa hili la udhamini. Kipindi cha nyuma kilimanjaro ndio ilikuwa inadhamini simba na yanga, na sasa sportpesa inadhamini timu hizo hizo mbili. Sijawahi ona duniani mdhamini mmoja anadhamini timu mbili katika ligi moja, ni uhuni na upuuzi wa hali ya juu.

Sijui huyu rais wa TFF kama yuko pale kwa maslahi mapana ya soka letu au ni kwaajili ya tumbo lake. Mnawapendelea simba na yanga na ndio maana ligi kwa ujumla wake ni mbovu na mitanzania ilivyo ni akili finyu imebaki kushangilia upuuzi.

Rais wa TFF inabidi apiganie maslahi mapana ya timu zote katika ligi pamoja na kuhamisisha wadau wajitokeze kudhamini timu mbali mbali.

Kwa style hii ligi yetu itabaki kuwa mbovu na kuendelea kuabishwa kimataifa.
 
NBC inakuja kuwa mdhamini mkuu wa ligi
 
kwani udhamini wa club mkataba anaingia tff au club husika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…