Habari. Mimi nina Probox na iko nzuri sana. Nimeinunua ikiwa na 38000km, kwa sasa ina 42000km. Nimesafiri nayo kwenda na kurudi kurudi Mrogoro, Dodoma, mara 2 bila tatizo na ni kwa matumizi ya familia siyo biashara. Gari ni zima kabisa. Kwetu TZ ni kama jipya. Kuna vitu kama viwili utatakiwa kubadilisha nadhani baada ya mwaka. Kama bado unahitaji tunaweza kuongea. Ila kama wachangiaji wengine walivyokueleza bei za Probox ndo hizo walizokutajia kama unataka gari zuri.