Wadau,
Hizi ni habari za kusikitisha, kuhusu yuke mtunzi maarufu wa military thriller books. Tom Clancy.
Mwandishi huyu amefariki Jumanne usiku kwenye hospitali ya Baltimore, chanzo bado hakijaelezwa, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Christian Post.
Nimeleta hili jukwaa atleast kwa ambao hawakufahamu kama mimi tujue kwa pamoja, kwa kuwa vitabu vyake vimetengenezewa game nyingi, nami ni mmojawapo wa mashabiki wake kupitia games zilizotengenezwa, mathalani;
Splinter Cell (toleo la mwisho likiwa Blacklist), Ghost Recon, Rainbow Six, nk. Pia ameandika The Hunt for Red October, ambayo Sean Connery ameigiza.
Poleni nyote wadau wa gaming. Najua ni mtu muhimu ametoweka. Peace.