Tofauti kati ya harusi na ndoa

mbinguni

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2013
Posts
2,784
Reaction score
1,078
Wakuu, kuna kitu nimekuwa nikijiuliza. Watu wengi wanapozungumzia kuoa au kuolewa, mara nyingi mawazo yanaenda kwenye harusi, mavazi mazuri, sherehe, wageni na shamrashamra za siku hiyo.

Lakini ukitazama kwa upande mwingine, harusi ni tukio la siku moja, wakati ndoa ni maisha ya watu wawili yanayoanza baada ya shamrashamra hizo kuisha.

Unaweza kuwa na harusi ya kifahari lakini ndoa yenye changamoto nyingi, na pia unaweza kuwa na harusi ya kawaida kabisa lakini ukawa na ndoa yenye furaha na amani.

Je, kwa mtazamo wenu, jamii yetu imekuwa ikiwekeza nguvu nyingi zaidi kwenye maandalizi ya harusi kuliko maandalizi ya maisha ya ndoa yenyewe?
 
Harusi ni shughuli ya shamrashamra inayoambatana na sherehe ila kinachotambulika ni ndoa hata kama usipofanya shughuli yeyote nje ya kanisa.
 
Ni harusi mwandishi

Tunasherehekea ni harusi ndoa ni kanisan na msikitini
 
Harusi ><ni fraha ,kula kunywa kwa sababu Mnaenda ku...t...MBA..na. kihalali.
Ndoa>kanisani au msikitini Watumishi WA Mungu wanawabariki mka....
t.om..ane kihalali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…