Malaria inasababishwa na plasmodium ambapo kuna aina kama nne za plasmodium wanaobebwa na mbu, kuna plasmodium vivax,ovale,falciparum na malariae.
MRDT ni Malarial Rapid Diagnosis Test inatumika kugundua uwepo wa malaria kwa haraka zaidi, inafanya kazi kwa kutumia antibody na antigen, antibody ni vilinda mwili vilivyopo kwenye seli, antigen ni visababisha ugonjwa.
Katika mRDT ni kwamba antigen za plasmodium zinaitikia sana kwa antibody ambazo ni aina fulani ya protein inaitwa HRP-II(Histidine Rich Protein-II), maabara tukichukua sample ya damu kama ina malaria tukiweka hio protein vikakutana vinatengeneza rangi mpya hivyo tukiona hio rangi tunasema mgonjwa ana malaria.
BS ni Blood Smear yaani tunachukua sample ya damu tunaweka kwenye kislide flan kama kichupa cha mstatili tunasmear kisha tunachungulia kwenye hadubini (microscope) tukiona plasmodium tunasema mgonjwa ana malaria.