Three Most Racist nations on Earth

Haha mkuu ungesema tu mnakua kama mbuni ungeeleweka ,eti mnaficha nyuso zenu shimoni ..........
 
Source: listovative.com/top-12-most-racist-countries-in-the-world/
4.Israel
5. Germany
6. Japan
7. Rwanda
8. Australia
9. UK
10. USA
11. Saudi Arabia
12. South Africa
 
Hivi kumbe ukiweka uccm pembeni unakua mtu wa kutumainiwa ?? kwa hili unastahili pongezi
 
Nashukuru kwamba umeelewa hata hapa kwetu hakuna demokrasia sasa unaposhupalia upinzani kosa lao ni lipi ?? Kwa maneno yako umesema demokrasia ni uongo mtupu na njia ya kupumbaza watu ili waendelee kutawala
 
Nashukuru kwamba umeelewa hata hapa kwetu hakuna demokrasia sasa unaposhupalia upinzani kosa lao ni lipi ?? Kwa maneno yako umesema demokrasia ni uongo mtupu na njia ya kupumbaza watu ili waendelee kutawala


Ndiyo maanake hata chadema kwenyewe hakuna Demokrasia ya kweli na ndiyo maana Lowasa alikaribishwa ndani ya masaa mawili akapewa nafasi ya kugombea uraisi hakuna mkutano wa kumchagua Mbowe kuwa Mwenyekiti wa chama, ameongoza Chama chaguzi tatu ambazo ameshindwa zote lkn bado ni Mwenyekiti wa Chama kwa hali ya kawaida alipaswa aachie ngazi kwa maana hakuna miujiza tena kama ameshindwa mara tatu na kuna watu wengine wanaoweza kujaribu lkn hilo haliwezekani kwa sababu hakuna wa kumuondoa kwani yeye na Mzee Mtei ambaye ni baba yake ndiyo Alfa na Omega wa siasa za chadema!
 
Sasa kama ndio hivyo kwa mfano wako huo mzuri ulivyoelezea racism ,ccm au chadema wanapata wapi mandate ya kuwanyoshea wenzao vidole ???
 
Sasa kama ndio hivyo kwa mfano wako huo mzuri ulivyoelezea racism ,ccm au chadema wanapata wapi mandate ya kuwanyoshea wenzao vidole ???


Hawapaswi kufanya hivyo kwa maana wote wawili wako sawa kwa namna moja ama nyingine na ndiyo maana unaona Bungeni likija kwenye swala la fedha Wabunge wote wa chadema, CUF, CCM n.k huungana na kutaka kulipwa fedha zaidi ngawaje wanajua fika kwamba maisha ya wananchi wanaowaongoza ni duni kupita kiasi lkn bado wanasema kwamba kwa kumnukuu Tundu Lisu anahitaji kulipwa milioni 300 kwa kuwa Ubunge umemtia umaskini, sasa ni nani alimlazimisha hata agombee Ubunge kama alijua utamtia Umaskini na hivi amegombea tena, sasa jiulize milioni 300 kwa hali duni wa watu wetu ukizimwaga kijijini zitasaidia watu wetu kwa kiasi gani?

Lkn wakisikia mambo complicated sijui escrow mara sijui capacity charges hapo ndipo mishipa inawatoka na kutaka waonyeshwe live kwenye TV na kuwaambia wananchi kwamba nchi yetu inaibiwa lkn wao wanavyoiibia nchi kwa kujilipa posho laki tatu kwa siku kiasi ambacho ndicho Mtz wa kawaida analipwa kwa mwezi tena mwenye familia ya watu 4 mbali na mshahara hawalioni hilo!
 
Sio kweli yapo mataifa ya north america watu wake in weusi
 
Nashukuru sana kwa majibu mazuri sasa naomba nikuulize ,kumbe likija kwenye swala la pesa au maslahi ya wabunge wote huwa kitu kimoja ,ila linapokuja swala kama hili la Zanzibar kila mmoja anaamini akijuacho ,wewe binafsi mtazamo wako juu ya Zanzibar ni upi ???
 
you couldn't be more true
japokua kuna ubaguzi kiasi, maana kuna cases za raia weusi kuuwawa na polisi kimakusudi, ila ikitokewa hukemewa sana
 
Source: listovative.com/top-12-most-racist-countries-in-the-world/
4.Israel
5. Germany
6. Japan
7. Rwanda
8. Australia
9. UK
10. USA
11. Saudi Arabia
12. South Africa
Rwanda??? tangia yale mauaji ya kimbari yafanyike, Rwanda wamekua watu wastaarabu sana, nadhani hii research imekosewa
 


Sina uelewa mkubwa sana kuhusu siasa za Zanzibar hasa kuhusu Katiba yao na Historia yao kwa ujumla na kipi hasa kilitokea mpaka kusababisha uchaguzi kufutwa, na je Katiba yao ilifwatwa au ilikiukwa na Je Mkuu wa Tume alikuwa na Mamlaka ya kuchukuwa uamuzi aliochukua au ala?
Hivyo inanibidi kwanza nijielimishe kuhusu hayo ili niweze kujua wapi na simama, na kwa bahati mbaya sana kwa sasa sijapata bado muda wa kulifanya hilo, hivyo kwa sasa sina jibu!
 
kwa wazungu wao even homophobic ni racism,,, ndio maana kwenye hiyo ramani hapo juu wameiweka Tanzania katika kundi moja na Russia...
homophobic na racism sio sawa bana
moja ipo based on sexuality nyingine ipo based kwenye skin colour
anyway kwani Tanzania kuna itikadi kali dhidi ya mashoga kihivyo? labda Uganda maana huko wanachomwa moto ila sijawahi ona hiyo hapa tz
ubaguzi dhidi ya mashoga hapa tz ni average na upo duniani kote hata America ambako kuna culture diversity kubwa
 
Nilijua tu lazima utatumia siasa kunijibu hilo swali hayo mambo sijui ya katiba au historia ndio cosmetic ulizosema kama wamarekani wapendavyo kufanya mambo ,
Kwa ufuatiliaji wako wa mambo unataka kuniambia hujasikia yaliyosemwa juu ya mamlaka ya Jecha aliyo nayo kufuta uchaguzi ?? Hujui katiba inasema nini ?? Tumewasikia wana ccm Kina Membe,Warioba wakisema hili kwa upande wao na pia tumesikia maoni ya wana ukawa kina Tundu Lisu, Maalim Seif,wasio na vyama ,wanasheria nk umesema kwa bahati mbaya hujapata muda wa kulifuatilia hilo kwa kifupi naweza kusema Zanzibar haipo kwenye priorities zako ,utakapo pata mda wa kufuatilia hili na pengine labda ni baada ya uchaguzi wenu wa marudio mliopanga kufanyika hapo mbeleni ,matokeo ya maamuzi yenu yawe mazuri au mabaya vipi utakua na la kusema ??
 


Nikiwa nimeshajielimisha vya kutosha nitakuwa kwenye nafasi ya kutoa hukumu yangu kwa sasa hivi naona kama naburuzwa tu huku na kule, na kama nilivyosema sifahamu mambo ya Zanzibar kiundani hivyo kwa mfano mpaka hivi majuzi sikujua kwamba Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ni tofauti na ya Muungano, mimi nilijua Tume ya Muungano ndiyo moja kote lkn kumbe siyo Zanzibar wana yao, hivyo basi ni muhimu kujielimisha kwanza ili niweze kufahamu nasimama wapi!
 
Ubaguzi hata hapa kwetu mwingi mno , makabila matatu yanaongoza kwenye masuala kijamii kama vile Elimu, kazi, Huduma za Afya Tembea uone la kwanza, la pili na Tatu.
 
Sina tatizo na wewe kujielimisha ila tatizo langu lipo kwenye muda ambao sio rafiki kwetu ,tuseme wewe upo kwenye nafasi ambayo utatakiwa utoe maamuzi ya nini cha kufanya baada ya uchaguzi kufutwa ,hii excuse yako ya kwamba unahitaji muda kujielimisha bado ingekua valid ??kumbuka hapo umepewa timeframe ya kuja na suluhisho,
Kwa kuanzia tu katiba ya Zanzibar imetoa siku 90 za kurudia uchaguzi endapo imebidi urudiwe ,mpaka tunavyoongea siku 90 zimepita kwa maana nyingine ni tumeizarau katiba ,hivyo conclusion yako isibase sana kwenye katiba au tume ya uchaguzi bali iwe tu kwenye utashi wa kawaida kabisa aliopewa mwanadamu na Mungu
 


Kama ningekuwa mtu wa kutoa maamuzi au kwenye nafasi yoyote ile kwenye hili swala ni lazima ningekuwa nafahamu yote ambayo siyafahamu leo hii!

Zanzibar kwangu mimi binafsi haijawahi kuwa muhimu ktk maisha yangu ya kila siku na ndiyo maana sielewi kwa sana mambo yao hata kufika huko nimefika mara moja tu hivyo ukiniuliuza sijui kuhusu Baraza la Wawakilishi au sijui Tume ya uchaguzi Zanzibar siwezi kufahamu ninachojua ni kile nilichofundishwa shuleni kwamba tunashea Jeshi, Mambo ya Ndani, Fedha na Mambo ya Nje baasi labda na kwamba asilimia kubwa ya Wananchi wa Zanzibar wale weusi wana asili ya kwetu yaani wanatoka Lindi, Kilwa, Mt, Tabora , Tanga mpka Kigoma n,k!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…