Mkuu,
Ya kweli haya? Si kwamba mnamuwekea maneno tu mtoto wa watu?
Kuna siku nilikuwa naongea naye mambo ya barabara za mikoa, mtu mmoja akauliza kuhusu daraja la Tanzanite.
Akaeleza jinsi Magufuli alivyo wa bully kulijenga.
Jamaa mwingine akamuuliza vipi, utagombea urais?
Aliruka vibaya sana akisema yeye kazi yake ya sasa ya uwaziri inamtosha sana, na tusimletee matatizo kwa kuongelea habari za urais.
Alijionesha kuwa mtu humble ambaye hana matamanio ya urais kwa sasa.
Huoni kwamba kumsema mtu wa hivyo kwamba ana njama za urais ni kumzushia tu?