Habari wana JF
Huku tukitafakari yaliyojiri 2012, napenda kuwaasa wanasiasa (najua wapo wengi tu humu) kujitathimini na kuangalia mipango ipi ya kisiasa waliyoifanya imeleta TIJA na ipi imeendelea kuudhi wananchi. Huku matatizo mengi yakiwa yamewaelemea wananchi ni wakati mwafaka wa kutumia busara sana na weledi wakati tukiangalia 2015. Siasa ni kama mpira wa miguu propaganda huwa inao mchango fulani tu ama kuleta wasiwasi, kujiaminisha au kuchafuana nk ( hata huko Marekani Barack Obama alipitishwa na chama chake cha Democrat kwa mara ya kwanza akiwa mgombea mwenye asili ya Afrika na kushinda ingawa hapo awali harakati za kumpitisha ziligubikwa na juhudi za kuwatisha tamaa wana Democrat wasimpitishe kwa kuwa hawezi kunadika sababu tu yeye ni mweusi.
Kwangu mimi propaganda ni upepo tu huwa unapita na watu husahau. Hivyo napenda kuwaasa wanasiasa hasa mnaopitapita humu pengine na viongozi wenu kuwa mtumie propaganda kwa umakini sana bila kusahau kuwa mwisho wa siku mambo yote huamriwa kwa kura (vote).
You can cheat some people for some time, but you can not cheat all the people all the time!!!!