Siku chache baada ya kukamilisha uhamisho wake wa kutoka timu ya Simba na kujiunga na Azam FC, kiungo mshambuliaji wa pembeni, Uhuru Seleiman Mwambungu, ameelezea mikakati yake mipya katika soka lake. Uhuru ambaye alishinda ubingwa wa Tusker Cup, akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar, mwaka 2009 na mataji mawili ya ligi kuu katika miaka yake mitatu na nusu kama mchezaji wa Simba, ameondoka klabuni, Simba uku akiwa si mchezaji muhimu kama mwanzo, mara nyingi amekuwa benchi na hata alipotumika ilikuwa ni kwa muda mchache tu. Tovuti ya kandanda, ilifanya mahojiano na kiungo huyu.
[TD="width: 64, bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"] Hali ilikuwaje kwa upande wako katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu, Tanzania Bara?[/TD]
[TD="width: 469"]Ilikuwa mbaya, sababu mimi ni mchezaji nisiyependa kubaki nyuma, yaani kukaa bila kucheza. Alafu timu inafanya vibaya, zaidi nilichukia kabisa mpira. Ila sasa nitarudi katika kiwango changu, na ningependa Milovan ( aliyekuwa kocha wa Simba) awepo Tanzania.[/TD]
[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Unadhani, Milovani ndiye alikuwa tatizo kwako? Labda wewe hukuwa ukitimiza majukumu aliyokuwa akitaka uyafanye na ukashindwa ndiyo maana akawa anakuacha nje?[/TD]
[TD="width: 469"]OK, ni hivi akili yangu haipo tena Simba na sitaki kuwaza kuhusu niliyokutana nayo uko ( Simba). Sasa naangalia ni vipi nitashirikiana na wenzangu katika timu yangu mpya ( Azam).[/TD]
[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Nini ambacho kilikufanya kufikiria kujiunga na Azam na si timu nyingine mara baada ya kuamua kuachana na Simba?[/TD]
[TD="width: 469"]Azam ni timu yenye malengo. Naamini itafanya vizuri, kikubwa nimeangalia nafasi ya kucheza katika mashindano ya kimataifa.[/TD]
[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"] Kama ni nafasi ya mashindano ya kimataifa, Simba pia itacheza na kama ni nafasi ya kucheza kikosini, mbona umekwenda kujirundika katika mkusanyiko mkubwa zaidi wa nafasi ndani ya Azam?[/TD]
[TD="width: 469"]Unapokuwa mchezaji, hilo si jambo la kujadili. Muhimu ni kuungana na wachezaji uliowakuta na kufanya kazi kwa pamoja. Mwalimu ndiye ataamua nani amtumie katika wakati upi.[/TD]
[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Kwa uzoefu wako wa kuzichezea timu kubwa kama Mtibwa na Simba na kushinda mataji, unadhani itakuwa hivyo pia kwa Azam?[/TD]
[TD="width: 469"]Naamini, Azam ni timu bora na imejipanga kufanya mapinduzi katika soka letu, hivyo kwa kushirikiana na wenzangu, nitafanya kila jitihada kuifanya, Azam kuchukua nafasi za juu katika mashindano ya Afrika na ligi kuu, ambayo naamini sasa utakuja kwetu.[/TD]
[TD="bgcolor: #F7F7F7"]
[/TD]
[TD="width: 469, bgcolor: #F7F7F7"]Timu nyingi zimeshindwa kuzipiku, Simba na Yanga na kutwaa taji la ligi, Mtibwa ilikuwa ni timu ya mwisho kufanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1999 na kurudia mwaka 2000, unadhani, Azam itazipiku timu hizo na kutwaa taji?[/TD]
[TD="width: 469"]Najua, Simba na Yanga ndiyo zinaisumbua, Azam, lakini mimi ninayo dawa yao na ninaijua.[/TD]