Mkuu Bavaria kwa wenzetu hakuna ujenzi ambao unafanyika bila kufanya assessment ya pollution. Kwenye hiyo barabara kama gari lako likitoa moshi unaweza kufungwa sana. Hapo mtoni kuna viumbe wanaoweza kudhuriwa na moshi wa magari.
Kaka aisee kama china wangekuwa waangalifu wa mazingira kiasi hicho nadhani wangekuwa mbali, kinyume chake ni kuwa jamaa wanaongoza kwa uchafuzi wa mazingira hewa ni chafu kupita maelezo,uchafuzi wa maji ni wa kutisha.Hii ni kutokana na ukuwaji wa viwanda wakajisahau kuhusu uchafuzi wa mazingira kwa hakika wanakazi kubwa jinsi gani watayaboresha.Ila ni fundisho pia kwetu ambao tunataka maendeleo ya haraka bila kujali uchafuzi wa mazingira na athari zake yatatukuta yanayowakuta wachina sasa.
Mkuu Bavaria yaani gharama zake zingekuwa juu vibaya sana maana ten percent ingewahusu sana hawa jamaa
Gharama ni kidogo sana na sijui tunashindwa nini maana barabara zetu zinajengwa hata hazijamaliza mwaka zishaanza kubomoka