Kwa jinsi ilivyo, na ukiangalia matendo na kauli zao wafuatayo the Hague inawahusu sana!
1. Chadema na mwenyekiti wao
Chama hiki hakijawahi kuhubiri amani au upendo. Kama yupo mtanzania amewahi kusikia neno upendo ndani ya kauli za viongozi wa chadema au neno amani likitumika in a positive way, naomba anirushie hiyo reference, naweza kubadili mawazo!
Lakini walipoanza tu kampeni walikuja na haya:-
a. Ccm ni wezi wa kura lkn sasa Yule mwizi tumemchukua "mr. Mwizi" yupo upande wetu. Kauli hii tata inatosha kufanya vyama vingine vikishindwa kujenga dhana kuwa ushindi wa chadema si halali Bali ni ule wa Mr. Mwizi
B. Kauli za kichochezi juu ya kutoiamini tume, wasimamizi wa kimataifa na vyombo vya usalama kuwa vinaibeba ccm! Kauli hizi maana yake ni kuwa hakuna mamlaka inayoweza kuwasimamia cdm isipokuwa chadema, Mbowe na Lowasa tu, huu ndio mwanzo wa mpasuko Mkuu kati ya polisi na wanachama au mashabiki wa CDM kiasi kwamba hadi sasa polisi inawawiu ugumu kudeal nao.
C. Kukaidi sheria, kanuni, taratibu na katiba ya nchi karibu muda wote. Hakuna SAA chadema wamewahi kukubali kufuata jambo kinyume na wanavyotaka wao hata pale walipokuwa wanajua kuwa wamekosea. Wamepindisha taratibu makusudi ili kuleta vurugu! Mfano. Kuvamia mikutano ya wenzao na kuleta ugomvi (rejea- Kyela) kuzomea ktk mikutano au kusimama barabarani na kumzomea mgombea wa chama kingine (rejea- Magufuli Mbeya, Dar na mkuranga) bila ya vitendo hivi kukemewa na chama. Kukaidi kanuni za uchaguzi za kutoa nafasi na Uhuru kwa wapiga kura kupisha vituoni kwa kutakuwa na misongamano hata baada ya mahakama kuamua vinginevyo! Kutoheshimu katiba ya Jamhuri ya muungano kwa kuidharau tume halali ya uchaguzi na kukaidi matokeo ambayo yanapewa nguvu kikatiba.
D. Kutoingilia kati matendo yanayofanywa na mashabiki na wanachama wake hasa ktk