View attachment 3558412
Story ya movie ya The Dutchman (2025) kuna namna fulani km imenigusa. Jinsi ilivyoanzia mpaka ilivyoishia.
Kuacha maelezo mengi km umeiangalia hii movie kuna kitu inasimulia kwa wale watu wanaopenda kulala lala na wapenzi tofauti tofauti wanapewa funzo.
View attachment 3558413
Huyo manzi unaemuona hapo juu ameigiza humo km Lula (demon) ambae alienda kumtongoza huyo mwamba hapo wakuitwa Williams, then wakaenda kufanya yao Williams akamkaza vizuri tu huyo demon lady.
View attachment 3558414
Kilichonishtua ni pale Williams alipomaliza kufanya mapenzi na huyo demon 'Lula' akaenda kujiangalia kwenye kioo na kuanza kujilaumu kwamba amefanya nini hiki? Hili ni jambo ambalo linawakuta wanaume wengi wakishamaliza kufanya ndio akili zinarudi.
Ghafla 'Lula' akawa km amekuja kwa nyuma ya Williams wakati huo Williams anajitazama kwenye kioo, sasa producer anatuonyesha kwamba yule 'Lula' (demon) ni Kibibi fulani hivi Kikongwe kilichojichokea balaa. Nikasema inamaana jamaa kafanya mapenzi na kile Kikongwe na kila akikiangalia anamuona ni Manzi fulani mzuri hatari, akageuka hapa producer anatuonyesha 'Lula' mzuri sio Kikongwe.
Paliponishtua ni hapo kwenye Kioo yule 'Lula' anaonekana ni Kikongwe balaa ila Williams alipogeuka nyuma anamuona Manzi fulani mkali hatari. Oya nimeshtuka sana.
Itafute na wewe ujithibitishie.
Ni nzuri ukiangalia huku unakunywa bia taratibu utajifunza kitu.