Mkuu hiyo hali niliishuhudia ktk Mechi ya Tanzania v Ivory Cost. Nilienda pale Steerz Posta nikaambiwa tiketi za 5000 zimeisha, kwa bahati nzuri nilichelewa. Ilipofika kama mida saa 11 lile gali linalouza tiketi likaondoka na mimi nikaamua kurudi zangu nyumbani, ghafla kuna jamaa akaniita nami nikaenda mpaka pale akaniuliza 'unataka tiketi'? Nikwambia ndio, akasema ya bei gani, nikamjibu ya 5000, akasema lete 7000 nikuuzie, hapo nikazama mfukoni na kumpa pesa, akanipa tiketi yangu nami nikarudi nyumbani. Yule jamaa alikuwa na tiketi zisipopungua 400 za 5000, sa sijui zingine alikuwa nazo za kiasi gani. Kwa kifupi, Maaskari na wauzaji wanajua mchezo unavyofanyika na wao ndo wanatumiwa zaidi.