Ligi yetu ya soka haina timu nyingi kama tunavoona nchi za wenzetu, sasa inakuwaje timu moja iwe imecheza mechi zaidi ya mbili kuliko timu nyingine? Majuzi kocha wa Toto African ya Mwanza alilalamika kwa kusema timu nyingine zina pungufu ya mechi tatu au nne, hii ni aibu sana kwa TFF. Ulaya pana timu nyingi kwenye ligi zao lakini huwezi sikia/soma pengo kubwa la mechi kati ya timu, sana sana itakuwa moja au mbili hivi.
Tuelezeni TFF soka letu mnalipeleka wapi?
..kazi yao kupeleka taarifa fifa kwa siri ili tufungiwe,eti fifa wamesoma kwenye vyombo vya habari,kibao kimewageuka fifa wamewaonea aibu kuwatimua kwa kuchakachua katiba bila mkutano,mtu kushinda rufaa bila kufika kusikiliza rufaa yake,aibuuu..
TFF kwa hili mmechemka, sasa hivi Kuna software ya kupanga fixtures au vijana hapa UDSM wanaweza kuwatengenezea else ni aibu ni lazima twende na wakati.