Tendwa mchochezi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Gazeti la Mawio la leo tarehe 25/7/2013 limepambwa na habari hii. Habari hii,ukurasa wa mbele kabisa,imechagizwa na nukuu nne za Mbowe,Tendwa,Dr.Slaa na Wakili Msomi Mabere Marando pamoja na picha ya kila mmoja. Ni vyema tukajionea nukuu hizi na kujadili. Kimsingi,suala kuu hapa ni 'mikwara' ya Tendwa kuifuta CHADEMA kwa kutaka kuimarisha ulinzi wa chama kupitia Red Brigade. Nukuu ni hizi:
Mbowe:"Unasemaje? Yule Bwana ni Mchochezi.Achana naye. Kuifuta CHADEMA unazungumzia kufukuza wabunge 49 waliopo Bungeni;madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000.Hili ni jambo ambalo haliwezi kuwazwa na mtu mwenye akili timamu."

Tendwa: '...chama cha siasa kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake ni kukiuka sheria za nchi."

Dr.Slaa: "Hilaz ote hizo tunazifahamu.Lakini kamwe hazitafanikiwa.Tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu."

Marando: "...kama analitakia mema Taifa hili,basi namshauri Bwana Tendwa aachane na ndoto zake hizi.Aache kutishia chama cha watu.Awaambie waliomtuma,CCM,kuwa matakwa yao hayatekelezeki."

Mwisho wa kunukuu. Nionavyo,Tendwa kama Mwanasheria kitaaluma anapaswa kuperuzi upya Sheria ya Vyama vya Sisa nchini na kujiridhisha kabla ya kutekeleza maagizo ‘ya kwenye simu,email,na vimemo'.Bado ana nafasi ya kufanya vizuri kama Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Sasa tujadili nukuu hizi.Karibuni!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Hiyo ni metamorphic rocks, tuendelee kujadili yetu. hayo tuwaachie wenyewe.
 
Makamanda mi mgeni ila mwana-CHADEMA nimemuona chriss lukosi youbue (mwenekiti CHADEMA londoni) je ni Chriss huyu ninae mwona anaiponda CHADEMA hapa JF au ni mwingine? Nijuzeni ili niwe namchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…