Naamini mko salama bin bukheri wa afya isipokuwa jemedari wetu alyeko Nairobi matibabuni, Mungu amsaidie.
Nimetamani tukumbushane tu juu ya yale matendo yetu tunayotenda kila siku. Sisi tuliopewa hadhi ya kuitwa binadamu tunauwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi ikiwemo kufikiri,kusema na kutenda. Hata hivyo ashukuriwe Mungu wa Mbinguni aliyevihifadhi vilindi vya mioyo yetu katika giza nene la siri,ni mpaka utakapozungumza ndipo watu watajua unawaza nini. Ndipo sasa Biblia ikatukumbusha kuwa huneni ila yaujazayo moyo wako yaani unayoyawaza.
Ubinadamu kwa mapana yake kuna mengi yatutofautishayo na wanyama ingawa kiuhallisia sote ni wanyama tu kwani tunazaliwa,tunakula,tunazaa,tunakufa..lakini ili uwe binadamu kwa heshima yake fikiri kabla ya kusema, kutenda. Samehe wanaokuudhi hasa kama maudhi yao hayana madhara sana, saidia unapoweza ila usitoe mpaka uhai wako kwa ajili ya sifa,kukosea tumeumbiwa ,omba msamaha, linda uhai wako na usalama wa Mali zako,nyenyekea ndugu yangu hujafa hujaumbika.Waheshimu wengine bila kujali hadhi zao. Na mwisho jiepushe sana na kulipa kisasi kwani yaliyopita si ndwele.
Ukifanya hayo machache na Mungu akuzidishie ufanye na kuzidi utakuwa na amani hapa duniani kuhusu mbinguni sijui.
Sent using
Jamii Forums mobile app