Ngoja niwape ushauri,
Aisee Voda ukitumia 4G ni hatari kwa afya yako, yaani ukiunga gb 1 ukizurura kidogo tu mtandaoni wanakutumia sms Yao kua umetumia 75% ya mb zako blah blah nyingi! Ukitumia 4G alafu Uplay video yaani Voda mb zao zinayeyuka kwa speed ambayo sielewi
Shida mojawapo niliyogundua let's say upo YouTube, unaplay video Ina dakika 10, afu unaitizama baada ya dakika 2 imeku bore unaiacha una click nyingine, aisee utaumia vibaya sana! Yaani kwa speed yao ya 4g unakuta wameshaidownload ile video online mpaka mwisho(Kuna kimstari keupe hua wanaonyesha) na MB zao unakuta washazikata kabisa, hii inamaanisha hata ukizima data bado una uwezo wa Kuangalia Hio video ya dakika 10 kutoka Hio dakika ya pili mpaka mwisho, maana inakua tayari imeshapakuliwa online na mb zinakua zishaenda, sasa ukiicancel ukaweka nyingine Hawa wapuuzi wanakua washakata MB za wewe Kuangalia dakika 10!
Ukifanya mchezo wa Kuangalia video nusunusu mfano upo insta unachek reels isipokufrahisha unachek nyingine aisee utaumia sana! Hawa wapuuzi watakupa stress za Mb, nadhani umenielewa!
Mimi nawasha 4G nikiwa na download ma file makubwa tu! Nje ya hapo naiset simu itumie 3g tu maana huku mjini Iko fasta sana sioni tofauti na mtu anayetumia 4g! Tangia nianze kufanya ivo naona mb zangu kidogo zinakakaa so haba! Nikiwaza wanaotumia 5g na huu ujinga wa Voda naona watakua na Hali Tete sana
Kuna kipindi wife nilimpa huu ushauri akawa mbishi, full kujiachia na 4g alafu alikua anapenda YouTube aisee alikua analalamika sana mara Voda wanakupendelea wewe, alivyokuja kuswitch to 3g anasema afadhali kidogo
Hebu mtu ajaribu hii mbinu afu a monitor matumizi yake ataleta mrejesho! Ila Voda ukijiachia na 4g ukitegemea Mb zitakaa utakula za USO
Sioni hata haja ya ku advance kwenda 5g kama wasipoboresha Bei za bando zao