Wasalaam,
Hili shirika la taifa la utangazaji sasa limekua kero tupu. Nimerudi home nimekuta wanaangalia habari TBC, asee nimeona kichefu chefu, mtangazaji sijui amevaa gauni, sujui dira aka dera, yaani unprofessionally kabisa. Halafu watangazaji wanafanya make up wapi sijui, maana hawavutii kuwaangalia hata chembe. Wanapaka vibaya hayo malips shine mixture wanja khaa yaani muonekano mbaya. Maripota nao hovyo tu
Mi wananijua sipendi kuangalia hii station hata kipindi kimoja. Nikaamuru itolewe mara moja. Ila nikaona nishee nanyi nilichokiona.
Baba Magufuli pitia na huku TBC, heshima ya hili shirika imepotea. Turudishie heshima ya shirika letu hili, tupende both radios and TVs zake. Kwa sasa ni aibu hata kuisimulia.