TBC ni CCM B, ukipata muda muda msikilize God Monyo wa ITV anavyoripoti pale Dodoma mjengoni. Anakupigia majumlisho kwamba wote waliochangia hawajikiti kwenye mswada bali CDM na Tundu Lisu. Lakini TBC wanazipamba zile ngonjera, mipasho, taarabu, makirikiri wa wabunge wa CCM na CUF. Eti mtu anadiriki kusema anawafundisha watanzania nini kipo kwenye mswada. Hii ni dharau kubwa kuwafanya WaTZ ni wajinga. Hawa jamaa wanajidai wakishaingia mjengoni basi tayari wameshapata akili kumbe ukilaza uko palepale. Achana na TBC ili usipate kichefuchefu. Wadhani kwa nini walimtimua Tido si alikataa kuipendelea CCM na kpindi chake cha MCHAKATO MAJIMBONI. Wale vijana pale TBC nawaonea huruma maana wanatangaza vitu ambavyo hawaamini. Yule Elisha Elia na kipindi chake cha Jambo ni aibu tupu anawaita pale akina Sendeka, Mod Rashid, na blabla zao. Namhurumia sana unakuwa msomi halafu vilaza wanakuelekeza cha kusema. Poleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee