JF DCTORS;
naomba msaada wenu, mimi nina vipele flani kisogoni, ni vile ambavyo watu wengi huwtoka wakati wakinyoa kwa wengi hupona baada ya muda mfupi, lakini kwangu haikuwa hivyo vipo mpaka sasa ni mwaka wa tisa na kila siku vinazidi kuongezeka, nmeshawahi kumuona dr. mmoja pale udsm akanambia kuwa haviponi hivyo nisijaribu kuvichezea tu havitakua, nkaona haitoshi nkaenda kairuki kuonana na specialist wa pale nae akanambia haviponi ila kuna dawa yeye anatengeneza ya ku-mix chemicals hiyo anaiuza yeye tsh. Laki tano na unatumia hiyo dawa kwa mda wa miezi sita mpaka mwaka mmoja,kwa uwezo wangu nikawa nmeshindwa kuipata.
Hivi vipele haviumu ila vinanikosesha uhuru na kuniaribia pozi mida flani hivi na kila siku vinaongezeka, nmeshawahi kumuona mtu akiwa na li-nyama likubwa kisogoni ambayo ni baada ya vipele hivi kufikia stage ya mwisho ya ukuaji, naomba msaada wenu jamani hata kwa dawa ya asili