Tatizo la misuli ya miguu kuuma

Tatizo la misuli ya miguu kuuma

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
5,362
Reaction score
4,125
Nimekuwa na tatizo hili kwa muda sasa, huwa linakuja na kuondoka lakini kwasasa naona linataka kuwa sugu. Kuna wakati nikiwa nimelala tu usiku basi misuli inakaza kwa nguvu na kuleta maumivu makali sana hasa misuli ya paja na ile ya nyuma ya ugoko, naomba ushauri wa kitabibu kujua hiki ni kitu gani na tiba yake ikoje. Mimi si mtu wa mazoezi sana na nikifanya mazoezi basi ni ya kunyanyua vitu vizito mara chache.
 
Pole sana mie huwa inakaza chini kabisa ya miguu na kwenye vidole na nikijaribu kuwa kama navinyoosha

kwenda chini kama hiyp pic inavyoonesha vinakakamaa kwa muda na nasikia maumivu makali kabla havijarudi katika hali yake,sijui shida ni nini mwanzoni nilidhani ni sababu ya viatu virefu nikaacha lakin bado hali ni ilie ile I hope kupitia thread nitapata msaada pia

beautiful-legs_2.jpg
 
tafuta asali changanya na mdalasini mchanganyiko wote hou weka kwenye maji ya moto,unywe asubuhi kabla ujapiga mswaki na wakati wa kulala ni dawa tosha
 
View attachment 133941

Pole sana dada, hata na mimi pia sometimes mpaka kwenye vidole huwa vinakamata lakini hasa mapaja na misuli ya mguu.
 
tafuta asali changanya na mdalasini mchanganyiko wote hou weka kwenye maji ya moto,unywe asubuhi kabla ujapiga mswaki na wakati wa kulala ni dawa tosha

Nachanganya kwa kiwango/kiasi gani? Na je nitatumia kwa muda gani mpaka nipone kabisa? Na je hiki kinasababishwa na nini?
 
nahisi tatitzo linatokana na upungufu wa madini fulani, Kwani mimi lilinitokea baada tu ya kujifungua na hali ilikuwa mbaya hasa nyakati za usiku, nilikuwa naogopa hadi kujigeuza, lakini baada ya muda likawa linapungua na mwisho nikatumia juice ya Alovera gel tatizo limeisha kabisa.Jaribu kuitumia hii mkuu.
 
Mm napata maumivu sa nyengine uwa nahic kama upande mmoja sio mwili wangu nikaambiwa nitumie vitamin b nimetumia lakn bado
 
Hii hali hata mm hunitokea najuaga ni pekeyangu tu kumbe tupo wengi.....mimi hasa mguu au nikijinyoosha usawa wa kifua had mbav aiseee natamanig hata kulia inauma sana
 
Pole sana mie huwa inakaza chini kabisa ya miguu na kwenye vidole na nikijaribu kuwa kama navinyoosha

kwenda chini kama hiyp pic inavyoonesha vinakakamaa kwa muda na nasikia maumivu makali kabla havijarudi katika hali yake,sijui shida ni nini mwanzoni nilidhani ni sababu ya viatu virefu nikaacha lakin bado hali ni ilie ile I hope kupitia thread nitapata msaada pia

View attachment 133941
Mm mwenyew nilijua viatu nikaacha ila bado ....pole sana
 
Jaribu Ku exercise miguu kila wakati yaani simple exercises hata ukiwa ume keti itakusaidia. Jaribu hivyo continuosly kwa wiki moja na utizame kama utapata kupindwa na miguu usiku. Ikiwa hakuna nafuu basi harakisha hospital kwani figo hua imechoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa na tatizo hili kwa muda sasa, huwa linakuja na kuondoka lakini kwasasa naona linataka kuwa sugu. Kuna wakati nikiwa nimelala tu usiku basi misuli inakaza kwa nguvu na kuleta maumivu makali sana hasa misuli ya paja na ile ya nyuma ya ugoko, naomba ushauri wa kitabibu kujua hiki ni kitu gani na tiba yake ikoje. Mimi si mtu wa mazoezi sana na nikifanya mazoezi basi ni ya kunyanyua vitu vizito mara chache.
Vipi mkuu tatizo lako liliisha au bado unasumbuliwa mpaka sasa?
 
Kuna mtu alinishauri kufanya mazoezi ya kukimbia na kuruka kamba atleast kwa mwezi mfululizo nione matokeo yake, kwakweli ilinisaidia sana kupunguza tatizo. Naweza kusema limepungua kwa kiasi kikubwa sana. Nafikiri pia uzito ulichangia sana kwa upande wangu maana tangu nilipoonza kufanya mazoezi na taratibu nyingine za kupunguza uzito hali imekuwa nzuri zaidi.
 
Okay good!
 
Back
Top Bottom