Mimi ni mkazi wa Kimara suca. Jaman hatujapata maji haya ya DAWASCO unakwenda mwezi wa pili sasa.
Napata mashaka na kujiuliza hivi 'maji sasa imekua ni bidhaa na si huduma tena kama zamani? Je hawa wanaojiita DAWASCO ni akina nani na wanafanya kazi kwa maslahi ya nani?
Wananchi ama wale wenye magari ya kuuza maji?
Ndugu zangu DAWASCO na wananchi wengine kwa mwendo huu tutafika kweli?
Mi naishi Kimara Mwisho huu ni mwezi wa4 sijaona bomba likitoa tone la maji....maji ya bomba yakitoka bill inakuja c zaidi ya 10000, lakini kwa sasa nalazimika kutumia zaidi ya Tsh 80000 kwa mwezi