Habari wakuu,
Naombeni msaada tafadhali,tablet yangu ya samsung galaxy imepata tatizo la kuonyesha battery empty na kuingia katika power saving mode ambayo inaifanya screen brighteness iwe very low na hivyo nashindwa kuitumia kabisa.
Tatizo hili hujitokeza mara baada ya kuitumia kwa dakika chache,kwa kuangalia video au kusomea hata kama nilikuwa nimeicharge 100% basi inajirudisha mpaka 0%.
Naomba msaada kwa anayejua jinsi ya kutatua tatizo hili,au anayefahamu fundi yoyote anayeweza kunitengenezea.
Niko Daresalaam