Nduguzangu katika Jamvi hili mambo haya ni ya kawaida maana siyo hapa tu ukiingia ulimwengu wa Mtandao zaidi wapo wanaoitwa webcam! Hawa huwa ni wezi wa kimataifa na wameliza wengi mara utaona msg kwenye barua pepe/face book yako mtu akijitambulisha kuwa ni mkimbizi mara ni binti pekee wa marehemu baba yake aliyemiliki kampuni au pesa nyingi na yeye ndo mrithi pekee. Usipende kumfuatilia zaidi usipokuwa makini utaishia kulizwa zaidi. Katika nchi yetu watu hawa hawapo bado katika nchi jirani wapo Rwanda, lakini zaidi wapo NIGERIA, IVORY COAST, MOROCCO, SUDAN na Ghana. Hapo mbeleni nitakuja niweke wazi nyaraka wanazopenda kutumia kuibia watu. Visit 449.com/ bittenus.com. Au safu majina kama haya Tamba dollo, Anabel coli hao ni baadhi ya wezi waitwao webcam.