Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,714
Dar es Salaam.
Hakimu mkazi mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Gabriel Mirumbe (54), amefariki
dunia katika Hospitali ya TMJ jijini hapa.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya
Kisutu, Isaya Arufani alisema jana kuwa Mirumbe alifariki dunia juzi
asubuhi.
Alisema Mirumbe alipelekwa
hospitalini hapo Jumapili usiku baada ya kuzidiwa na maradhi yaliyokuwa
ambayo hakuyataja.
Hakimu huyo ambaye ni mzaliwa
wa Tarime mkoani Mara, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa nyumbani kwake
Mbezi Salasala.[FONT=courier
new]
[/FONT]
Enzi za uhai wake, Mirumbe
alifanya kazi katika Idara mbalimbali za mahakama katika mikoa ya
Kigoma, Tabora na Dar es Salaam. Akiwa mkoani Dar es Salaam, Mirumbe
alifanya kazi katika Mahakama Kuu, Mahakama ya Kivukoni, na ya
Kinondoni.
Akiwa katika Mahakama ya Wilaya
Kinondoni mwaka 1999, alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela
mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila
kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi.
Mpaka mauti yanamfika, alikuwa
miongoni mwa mahakimu waliokuwa wakiunda jopo la kusikiliza kesi ya wizi
wa Sh6 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa)
inayowakabili wafanyabiashara Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza.
​Chanzo:
Mwananchi
Hebu kuweni makini katika kuandika habari, mnakimbilia wapi? mnashindana na nani? Hebu tazameni hii sentesi hapa chini ipo katika paragrafu ya tatu hapo juu
Alisema Mirumbe alipelekwa hospitalini hapo Jumapili usiku baada ya kuzidiwa na maradhi yaliyokuwa ambayo hakuyataja.
RIP Hakimu
Mkuu ndo wandishi wetu hao tuwavumilie tu! Kazi tunayo kwa kweli!
Hebu kuweni makini katika kuandika habari, mnakimbilia wapi? mnashindana na nani? Hebu tazameni hii sentesi hapa chini ipo katika paragrafu ya tatu hapo juu
Alisema Mirumbe alipelekwa hospitalini hapo Jumapili usiku baada ya kuzidiwa na maradhi yaliyokuwa ambayo hakuyataja.
RIP Hakimu
Una lako jambo unataka kumlisha maneno mwandishi sio.
Sema wewe amaugua nini.
Alale anapostahili Hakimu wetu..
Wewe ndo wale wale, sasa hicho ndio kiswahili gani cha "....maradhi yaliyokuwa ambayo hakuyataja" mkirekebishwa hamtaki, mkipigwa chini mnalalamikaUna lako jambo unataka kumlisha maneno mwandishi sio.
Sema wewe amaugua nini.
Wewe kichwa nazi tena koroma!!! Ina maana umesoma habari yote haujakiona alichokionesha huyo mdau? Na wewe ndo hao hao tu, sijui huwa mnaandika habari huku mkiwaza michepuko? Shame on you kichwa koroma!!!!!Una lako jambo unataka kumlisha maneno mwandishi sio.
Sema wewe amaugua nini.