Tanzania's Unusual Immigration Case


Wale waimbaji walishasema kwenu kuzuri sasa mbona hampataki? Rudini mkaijenge nchi yenu acheni kung'ang'ania nchi za wezenu.
 

Hauwezi kutambua uraia wa mtu kutokana na Jina lake, shirikisha ubongo wako kidogo
 
Kagame's arrogance is to blame for all this. Tanzania fears another M23 in there region. Unfortunately the game hurts some few innocents.

This is like a misguided missile landing in civilian areas, causing casualties.

But for those who have lived illegally in Tanzania, why should they complain and demand legal eviction. Who is paying for the eviction exercise? One has to stop and think. I am not saying that these cattle and other properties are to pay for the exercise, but it is also possible they come with nothing, they depart with nothing, if that is true at all.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Wale waimbaji walishasema kwenu kuzuri sasa mbona hampataki? Rudini mkaijenge nchi yenu acheni kung'ang'ania nchi za wezenu.

Acha kurukia mambo usiyoyajua, wale waimbaji wimbo wao hauhusiki na huu ujinga.
 
Acha kurukia mambo usiyoyajua, wale waimbaji wimbo wao hauhusiki na huu ujinga.

Kumbe unajua ni ujinga kuingia nchi za watu bila utaratibu? Mtakoma rudini kwenu. Mwisho wa kuifanya Tanzania shamba la bibi unakaribia.
 

Why do not the Government legalize their stay? the story here is mentioning someone who was born by naturalized parents right here in Tanzania since the Mwalimu's Regime, where was the Government all that time? all to come and falal on innocent being because of nonesense misunderstanding between two arrogant and insensitive presidents to the wellbeing of humanity.

those guys, whether rwandese or Tanzanians they have humanity right to live where ever they want without regard of nonsense national borders.
 
Tatizo kubwa la Wanyarwanda walisahau kwamba wamekaa kwenye nyumba ya kioo hivyo hawaruhusiwi kurusha mawe. Wameanza wao kurusha mawe kwa watanzania kwa kuwatukana matusi ya nguoni na aliyefanya hivyo ni kiongozi wao na wote wakashangilia sana, wakasahau fadhila waliyopewa. Kama hiyo haitoshi, wakajiunga na wakorofi wengine eti kuitenga Tanzania kwenye jumuiya ya EAC na kusitisha matumizi ya bandari ya DSM wakifikiri wanawakomoa WATZ. Leo mnakuja na story kibao ukweli unabaki pale pale wewe ni mhamiaji haramu haijalishi umekaa hapa miaka mingapi na umefanya nini. Zaidi ya yote, walipewa muda wa kuondoka kwa hiari sasa wao walitegemea nini? Kuwa na cheti cha kuzaliwa Tanzania haimaanishi wewe ni mtanzania, bali ni asili ya wazazi wako. Tanzania mnaichezea sana mara Malawi wanataka ziwa nyasa lote liwe lao na wako tayari eti hata kwa vita. Haya sasa wanyasa wote haramu kwenu, wanyarwanda wote haramu kwenu, wakenya na waganda wote haramu kwenu. Hivi nyie hamjui kwamba Tanzania haina cha kupoteza. Embu na nyie wafukuzeni wahamiaji haramu watanzania kwenye nchi zenu muone kama wapo au wanazidi hata 10. Mmerusha mawe hali mnakaa kwenye nyumba ya kioo sasa tanzania imegusa tu hicho kimoja cha wahamiaji haramu ambacho kimsingi ni haki kama nchi kelele chungu mbovu. Mara mnataka bunge la EAC lisikutane Arusha tu hali kwamba pale Arusha ndipo kwenye ukumbi maalum uliojengwa wa bunge hilo. Kwa kuonyesha jeuri yenu mkaungana wote mkatoka nje mkimshinikiza spika w abunge la EAC akubali ajend ayenu na mkawaacha ukumbini watanzania wanashangaa. Hatimaye ajend ayenu ikapita mkifikiri mnaikomoa Tanzania hali ni kuzidi kuongeza gharama zisizo za lazima kwa jumuiya. Ni wakati umefika sasa kila mtu kwao. Huo ndio ukweli wenyewe. KAMA NI EAC KUVUNJIKA ACHA IVUNJIKE TANZANIA ITAENDELEA KUWEPO DAIMA DUMU. TUONE SASA MKIANZA KUPIGANA MTAKIMBILIA WAPI?
 
Kumbe unajua ni ujinga kuingia nchi za watu bila utaratibu? Mtakoma rudini kwenu. Mwisho wa kuifanya Tanzania shamba la bibi unakaribia.

Maofisa wa Uhamiaji wako kila kona nchi hii, walikuwa wapi muda wote huo? Ustaarabu ambao watanzania wamekuwa wakijivunia kwa miaka nenda rudi, tena hata ile historia ya kusaidia majirani wakaribu na wambali katika kujipatia uhuru wa bendera kutoka kwa wakoroni uko kwenye majaribu makubwa kwa matendo yanamna hii.
 
Mkuu acha kupotosha Jean Claude ni jina kifaransa, Tanzania angeitwa John Claud au Yohana Claudio kwa hiyo hilo jina ni tosha kabisa kuwa huyu siyo mtanzania kaka
 

Mambo ya Kagame kurushiana maneno na Jakaya yalitokana na namna Kagame kushughurikia tatizo la waasi wa serikali yake mwenyewe, hata kama kuna m23 issues, sio fair kwenda kuwakurupua watu wengine, Kama ni swala la wahamiaji haramu nchi hii wamo maelfu kwa maelfu, achilia mbali wote hao wako hapa katika kutafuta ama ridhki ama kuishi kabisa kama hao wanaodharirishwa sasa na askari wetu.

Hao watu hawana uhusiano wowote ule na siasa za East Africa, na wala Tanzania kutengwa sio dhambi, by the way tumekuwa tukidai hatutaki kuingia kwenye federation wala kitu chochote sababu tunaogopa kuibiwa ardhi na nini sijui, kwa nini kuwatwisha watu wengine hasira zetu.
 
hii oparesheni kimbunga lazima itende haki,tusije tukawafukuza wakina YUSSUF,mnao soma biblia nadhani mnakumbuka hii story
 

Umeishawaona watu wenye asiri ya rwanda wanapigana na wacongoman wa kinshasa? au kwa vile kwenye mipaka yetu hapajachafuka?
 
Tunamshauri rais wa tanzania aongeze nguvu na kasi hawa kizazi kijacho wanaweza kuanzisha goma na kivu nyingine hapa kwetu . Sasa tukaze buti kusafisha hii mbegu mbaya ikiwezekana na watoto waliwazaa hapa tz nao waondoke ndiyo solution permanent otherwise our descendants will suffer from the politenes in disguise we are trying to portray towards the illegal immigrants. There is no good in keeping illegal intruders. Naunga mkono mia kwa mia hawa wanapenda kujitanabaisha kwa ututsi na kuona kama wabantu waliletwa duniani kwa bahati mbaya vile. Waondoke hatuwataki
 

Kwani ulikuwa hujui kuwa wema una mwisho? Rudi kwenu Rwanda ukajenge nchi yako acha kutafuta huruma ya watanzania.
 
hawa wanajua stahili ya majina ya Tanzania ila wanajifanya kung'ang'ania kifaransa sasa wasiduwae huu uzalendo wakutumia majina ya kifaransa unatoka wapi kwa mtanzania aiyejua kifaransa acha huo utamaduni wao. bila shaka huyo ni mhamiaji haramu aondoke tu. hata kama mipaka tuliwekewa na wakoloni. hapa baadae kilizuka kizazi cha mauaji katika mataifa haya madogo na sisi watz hatuja pata serious cases za geneocide. kwahiyo mbegu hatuitaki ibakie hapa . tunamuona jirani yetu anavyoshindwa kuendeshwa nchi kutokana na hawa wanaojitafutia maisha. kwahiyo there is no more solution than chasing them out i thin k this is the best choice of all choices we have around us
 
Hawa tunaowaita "illegal immigrants" wametukosea nini?
Matatizo ya kila siku ya Mtanzania kwenye kuwasiliana.

Hawa tunaowaita wahamiaji haramu wametukosea nini, wametokusea kwa kuwa wahamiaji haramu!

Ni aibu kwa nchi kama kama yetu. Kwa nini sisi? Tutajie nchi moja duniani ambayo ina mipaka ya wazi, unayoweza kuingia na kukaa na kutoka na kuingia tena na kufanya unavyotaka. Sasa sisi nchi ya nani, Mama Theressa?

Mkizidi mahala shurti mfukuzwe, hususan mkionekana hamna shukurani. Afrika Kusini tulipigana kuwakomboa, tulipozidi tulifukuzwa kwa fimbo mitaani!
 
hapo ni mwanzo tu bado tunaanza kufuatilia wale wafanyakazi haramu. tafadhali mtukufu rais uandae jeshi lingine la kupita maofisini kukagua wafanyakazi haramu waliopenya milango ya dhahabu bila kugundulika na vyombo vya usalama. nasikia wapo tele hadi katika sekta nyeti kama ikulu. sasa juzi wakti kamanda anaendelea na zoezi baadhi ya vigogo ndugu wa wahamiaji haramu walianza kumpigia simu kamanda . nafikiri hao waliompigia simu tuanze nao hao kwa kuwapekua tujue kama ni watanzania kweli au la vinginevyo zoezi hili lifannywe kwa weledi na msingi ya uadilifu ambao Jeshi letu limeweza kuonesha mpaka sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…