Tanzania yetu

hard core

Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
46
Reaction score
28
TANZANIA YETU

1. Kwa miaka 51 hii inchi imeongozwa na CCM peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.

2. Tz ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square yani sawa na uchukuwe Denmark,France, United kingdom(uk),Netherland,Ireland ujumlishe zote kwa pamoja.

3. Tz ni nchi ya tatu kwa uzalishaji dhahabu afrika na ipo top 20 duniani.

4. Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee inayozalisha madini ya Tanzanite duniani.

5. Tz ina migodi pia ya Almasi,Uranium kule Dodoma ambao unamilikiwa na Warusi,chuma kule lganga na mchuchuma mbeya ambacho kimechanganyika na Tatinum ambacho kilo 1 ni karibia laki moja. Tz ina hifadhi ya kubwa ya makaa ya mawe kule Mbeya

6. Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424 kilometers bahari inaleta fursa za usafirishaji,uv uvi,utalii na nyinginezo.

7. Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani baada ya Marekani na Uturuki.

8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine madogo mengi.Maziwa matatumakubwa yako kwenye kumi bora za ukubwa duniani na Maziwa makubwamatatu yote yapo Tanzania Ziwa Victoria ni la tatu kwa ukubwa duniani(la kwanza Afrika) na Ziwa Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika) na la kwanza kwa
kuwa na kina kirefu duniani.Ziwa Nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani(ni la 3 afrika).

9. Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni Mto Kagera,Mto Ruvuma,Mto Rufiji,Mto Wami,mto Maragarasi,Mto Mara,Mto pangani,Mto Mara,Mto Gombe,Mto Mweupe wa Nile na ina Mito midogo mengi kama mto Kilombero,Mto Mbemkuru.

10. Tz ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani.

11. Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga maarufu duniani Serengeti na mlima mrefu kuliko wote Africa Kilimanjaro.

12. Tz ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga makubwa kama matetemeko ya ardhi,magonjwa kama Ebola,mafuriko na vimbunga au ukame.

13. Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho nnchi za Africa zimekikosa AMANI kwa miaka yote 51 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya wenyewe kwa wenyewe.

14. Tz ni nnchi ambayo imepakana na nchi (Uganda,Rwanda, Burundi,Zambia,Malawi,Drc congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu.

15. Tanzania imechaguliwa kama Nchi ya kwanza Afrika kwa kuwa na vivutio vinavyohamasish a Utalii. Nchi zilizokuwa kwenye tano bora ni Tanzania, Botswana, Afrika Kusini, Kenya na Zambia.

16. Tz ndiyo nchi ya kwanza Africa kuwa na maji mengi yaio na chumvi yaliyokuwakwenye uso wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa na mito na Maziwa mengi na kupitiwa na Bonde la ufa.

17. Nadhani kila mtanzania anajua juu ya sifa ya Tanzania kwenye swala la kuwa na ardhi ya rutuba inayofaa kwa kilimo.

Pamoja na sifa zote hizi lakini Tz ni nchi iliyokwenye kundi la nchi maskini duniani ambao asilimia kubwa ya raia wanaishi chini ya dola moja.

TAFAKARI
 
hyo ndio Tanzania mzawavuv wa ngarawa mgen ameket na kombe la kahawa,,,,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…