Baada ya miaka kadhaa tutakuwa kwenya nafasi nzuri ya kuwa nchi ya viwanda .
Umeongea point sana.tatizo lililopo ni kwamba huu mpango mzima wa viwanda haujaeleweka kiuhakika kwa watendaji na viongoz wengi serikalini.kuna ule usemi " the devil is in the details".kushindwa au kufanikiwa kwa kitu chochote kile kipo katika details.Watanzania tupo tayari kabisa kuanzisha na kuendesha viwanda na hasa vidogo vidogo visivyohitaji technology kubwa. Tatizo ni serikali kutoipa kipaumbele cha kutosha sekita hii. Viongozi na wanasiasa wanatuhadaa sana Watanzania, maneno yao majukwaani ni tofauti kabisa linapokuja suala la utekelezaji wa wanachokihubiri.
Mheshimiwa Raisi ana dhamira nzuri sana ya kuanzisha na kuendeleza viwanda, lakini viongozi ( wasaidizi) alio nao ndio wanaomuangusha. Wengine wanapiga porojo majukwaani lakini ukiwafuata maofisini si msaada sana sana wanakumbatia wawekezaji wa kigeni kuliko sisi wazawa.
Kipaumbele kikubwa kinatolewa kwenye viwanda vikubwa, viwanda vidogo vidogo ambavyo Watanzania wazawa wanao uwezo wa kuvianzisha havithaminiwi badala yake serikali badala ya kuvisaidia kwa kutumia watalaam wake vifanye nini ili viweze kukua na kufikia viwanda vya kati badala yake wanavikandamiza kwa kuvitoza utitiri wa kodi na kuvifungia kwa kukiuka taratibu.
Nina mfano mdogo, siku chache zilizopita nilimsikia mkuu wa mkoa wa DAR ES SALAAM, mheshimiwa Paulo Makonda akisema juu ya ujenzi au uwekezaji kwenye viwanda vidogo vidogo katika mkoa wake, kauli hii ilinihuzunisha sana na ndiyo inayonipelekea nimesema kuwa VIONGOZI wetu hawana dhamira za dhati kwenye uanzishaji na uendeshaji wa viwanda na hasa vidogo na vya kati. Mimi binafsi nilikuwa na kiwanda kidogo cha kusindika chakula. Kiwanda ambacho kilikuwa kina vibali vyote vinavyotakiwa. Kiwanda hiki kilikuwa katika mkoa wa DAR ES SALAAM. Kiwanda ambacho nilikianzisha kwa mtaji wa kudunduliza na kimefanyakazi toka mwaka 2010 hadi 2016 kilipobomolewa kwenye mazingira ambayo ni tata. Nasema mazingira tata kwasababu hakukuwa na wala hatukuwahi kupewa taarifa kuwa kiwanda kiondolewe, lakini tulipewa dakika tano za kuhamisha mali na mashine na kikabomolewa. Malalamiko ya kilichofanyika niliyafikisha ofisini kwa mkuu wa mkoa mheshimiwa Paulo Makonda. Lakini hakuna chochote kilichofanyika niliishia kuzungushwa tu.
Hapa ndipo ninapohoji dhamira safi ya viongozi wetu ya kuhamasisha wananchi kuanzisha viwanda. Kama vilivyopo havisaidiwi hivyo vipya vitaanzishwaje?. Baada ya kiwanda kuvunjwa nimebaki na mashine ambazo zinazidi kuharibika kwa kukaa tu bila kufanyakazi. Kwa sababu mtaji wote uliharibiwa.
Maneno ya mheshimiwa Rais Magufuli kuwa Tanzania ilitakiwa iwe donor country, ni Watanzania wachache tunaomuelewa, ni maneno ya kweli, lakini kuna watu tuliowakabidhi dhamana ya kututumikia ndio wanaotuangusha na ndio wanaotupeleka kwenye dimbwi la umasikini mkubwa. Nilitembelea China mwaka 2015, ziara yangu ilikuwa ni kutembelea viwanda vidogo na vya kati moja ya mambo ambayo nilijifunza ni baadhi ya bidhaa ambazo zikija huku kwetu zinauzwa bei kubwa na wakati hazihitaji technology kubwa kuzitengeneza kiasi kwamba hata sisi hapa tunaweza kuzitengeneza na tukauza hata kwenye nchi zingine za Africa. Na tungetengeneza ajira kwa Watanzania wenzetu. Nikiangalia namba ya vijana wanaomaliza kwenye vyuo vikuu yetu asimilia kubwa wanasubiri serikali iwaajili. Na viongozi waliopewa dhamana hakuna ubunifu wowote wanaoufanya wa kuondoa changamoto kama hizi. Tunaojitahidi kujikwamua kidogo ndio hivyo tena tunarudishwa nyuma hatua zaidi ya 100.
Ninapenda kumalizia kwa kusema haya. 1. KWA VIJANA na hasa wasomi wetu mnaomaliza na mlioko vyuo vikuu tumuunge mkono mheshimiwa Rais kwa kufanyakazi na mtumie elimu mlioipata na mnayoipata kwa kubuni miradi ya uzalishaji mali kwa kutumia technology rahisi ili miradi hiyo iweze kuajili kundi kubwa la vijana wa Taifa hili. Pia tumieni mitandao ya kijamii kwa kuweka mada zinazolenga na kuhamasisha vijana kujitambua na kutumia muda wao mwingi katika kujadili namna na kupeana fursa za kujikwamua ki uchumi.
2. KWA VIONGOZI mliopewa dhamana na hasa viongozi vijana, tutendeeni haki Watanzania kwa kutatua matatizo yetu na hasa haya uzalishaji mali, viongozi mlio wengi mkishapata madaraka/ vyeo mnakaa mbali na wanachi na matokeo yake mnageuka kuwa watesi wetu. Watanzania tupo tayari kuwekeza kwenye viwanda ila baadhi ya sera ni kandamizi, baadhi ya taratibu zinaingiliana kati ya wizara moja na nyingine na kupelekea utitiri wa Ada, tozo, na kodi kuwa kubwa kwa mwekezaji.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais wetu. Amina.
Mkuu;
Kutokana na upinzani mkubwa wa kisiasa, hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 5 ya kikatiba. Mwenye mawazo kama yako anatamani ayaweke hayo mazingira mazuri ila ajaye naye anayafuta yote kama kwamba ni chama tofauti kimeingia madarakani. Naye anaanzisha vya kwake. Mwingine anaviuza viwanda, nyumba za serekali utadhani hakuna tena kiongozi atakaa aje hapo kuongoza. Yaani, hii ni mawazo vurugu tu. Siku zinapita, miaka, unakuta upo pale pale hivyo kuwalaumu wapinzani huku huna cha kuonesha.